STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 3, 2013

Yaya Toure ndiye Mchezahi Bora Afrika wa BBC

KIUNGO nyota wa Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast, Yaya Toure amechaguliwa kuwa mchezaji bora Afrika wa tuzo ya BBC 2013.
Toure amenyakua tuzo hiyo akiipokea toka kwa Mzambia Christopher Katongo aliyeinyakua mwaka jana.
Kiungo huyo ametwaa tuzo hiyo kwa kuwapiku Pierre-Emerick Aubameyang, Victor Moses, John Mikel Obi na Jonathan Pitroipa .
KUTOKA KUSHOTO; AUBAMEYANG, PITROIPA, OBI, MOSES NA YAYA.
Yaya mwenye miaka 30, ameiambia BBC kuwa: “Nimeteuliwa kwa miaka minne bila ya kushinda, safari hii ni mara ya tano na nimeshinda, ni kitu cha aina yake.”
 “Nina furaha kubwa kufanikiwa kushinda tuzo hii kubwa na ninatoa shukurani zangu kwa waandaaji.

"Najua kuna wachezaji wengi bora barani Afrika mfano kama Aubameyang, Pitroipa, Mikel, Moses, Salomon Kalou, Gervinho na wengine wengi lakini leo nimeshinda.”

Yaya pia alilisifia bara la Afrika kwa kuendelea kuzalisha vipaji na mpira wake kuendelea kupiga hatua.

No comments:

Post a Comment