SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) linatafakari hatua zaidi za kinidhamu dhidi ya
wachezaji wawili wa kikosi cha Twiga Stars walioondolewa kwenye timu
hiyo na Kocha Rogasian Kaijage.
Kocha
Kaijage aliwatimua kambini wachezaji Mwapewa Mtumwa na Flora Kayanda
kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu wakati Twiga Stars ikijiandaa
kwa mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya
Zambia.
“TFF tunaunga mkono hatua iliyochukuliwa na Kocha Kaijage dhidi ya wachezaji hao wakongwe wa Twiga Stars, kwani katika shughuli yoyote ile inayohitaji ufanisi nidhamu ni kitu cha kwanza,” imesema taarifa ya TFF.
Twiga Stars itacheza mechi za mchujo za michezo ya 11 ya Afrika (All Africa Games) ambayo itafanyika mwakani nchini Congo Brazzaville.
No comments:
Post a Comment