STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, March 4, 2014

Young Hassanally kuzindua Nyongo Mkaa na Ini

* Uzinduzi kufanyika Ijumaa Travertine Hotel
* Khadija Kopa, Jokha Kassim,Mwanahawa Ally ndani
Muimbaji Hassani Ally 'Young Hassanally'
Mwanahawa Ally naye atakuwepo ukumbini kumsindikiza Young Hassanally
Khadija Kopa (kushoto) naye atakuwepo Travertine Hotel
MALKIA wa Mipasho nchini, Khadija Kopa, Mwanahawa Ally na Jokha Kassim wanatarajiwa kusindikiza uzinduzi wa albamu mpya binafsi ya muimbaji nyota wa muziki wa taarab nchini anayeliimbia kundi la King's Modern Taarab, Hassan Ally 'Young Hassanally'.
Uzinduzi huo wa albamu hiyo inayofahamika kwa jina la 'Nyongo Mkaa na Ini' utafanyika siku ya Ijumaa kwenye ukumbi wa hoteli maarufu iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na MICHARAZO, Young Hassanally, alisema mbali na waimbaji hao mahiri nchini, pia uzinduzi huo utasindikizwa na kundi la King's Modern Taarab maarufu kama 'Wana Kijoka'.
Hassanally, alisema ameamua kuwashiriki wakali hao katika uzinduzi wake ili kuunogesha na kuwapa burudani mashabiki wa muziki wa mwambao.
"Siku ya Ijumaa natarajia kuzindua albamu yangu ya pili mpya iitwayo 'Nyongo Mkaa na Ini' ambapo nitasindikizwa na wakali wa muziki wa mwambao Afrika Mashariki na Kati, Al-hanisa Khadija Kopa, Mwanahawa Ally 'B52' na Jokha Kassim pia kundi langu la King's Modern litakuwapo ukumbini Magomeni kunisindikiza," alisema.
Hiyo ni albamu ya pili binafsi ya staa huyo baada ya awali kuzidnua albamu ya 'Aibu Yao Aibu Yetu' na  aliongeza kuwa maandalizi yote ya uzinduzi huo yamekamilika na kwa sasa kinachosubiriwa na siku ya uzinduzi huo ili mashabiki wapate burudani, huku akitaja viingilio ni Sh. 5000 tu kila kichwa.

No comments:

Post a Comment