STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, March 5, 2014

Taifa Stars dimbani leo Namibia bila Samatta, Ulimwengu

Taifa Stars
Mbwana Samatta (kulia) atakayelikosa pambano la leo nchini Namibia

TIMU ya Taifa (Taifa Stars), itawakosa nyota wake wanaocheza soka nje ya nchi katika mechi ya kirafiki ya Kimataifa dhidi ya Namibia itakayochezwa leo kwenye Uwanja wa Sam Nujoma jijini Windhoek nchini humo.
Hatua hiyo inakuja baada ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) kushindwa kupata usafiri wa uhakika wa kuwarejesha ndani saa 24 katika klabu yao, washambuliaji Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu wanaoichezea TP Mazembe ya DR Congo pamoja na Mwinyi Kazimoto anayeichezea Al-Makhiya ya Qatar.
Stars ya TFF (iliyoteuliwa na shirikisho hilo badala ya kocha), iliondoka nchini juzi alfajiri ikiwa chini ya Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa shirikisho hilo, Salum Madadi, aliyeshika kwa muda nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mdenmark Kim Poulsen, ambaye alitimuliwa wiki iliyopita.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, aliliambia NIPASHE jijini Dar es Salaam jana kuwa, Stars itashuka dimbani bila ya wachezaji wake wanaosakata kabumbu la kulipwa nje ya nchi, Ulimwengu, Samata  na Kazimoto.
Alisema wachezaji hao wanakosekana baada ya TFF kukosa ndege ya kuwarudisha katika timu zao ndani ya saa 24 baada ya mechi hiyo kumalizika kama Kanuni za Fifa zinavyoelekeza.
"Ndege tulizopata zinapita Nairobi kwenda Lubumbashi Machi 8, wakati Samata na Ulimwengu wana mechi muhimu ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwishoni mwa wiki," alisema Wambura.
Aidha, Wambura alisema Stars itawakosa wachezaji Hassan Mwasapili na Edward Charles ambao wamekosa hati za kusafiria (passport).
Kutokana na kukwama kwa nyota hao, Stars sasa imebaki na wachezaji 15 wakiwamo makipa Mwadini Ally (Azam) na Shaban Kado (Coastal) aliyeitwa kuziba nafasi ya Ivo Mapunda (Simba) aliyefiwa na baba yake mzazi wiki iliyopita.
Mabeki ni Erasto Nyoni, Said Moradi na Aggrey Morris (Azam), Abdi Banda (Coastal) na Michael Aidan (Ruvu Shooting), wakati viungo ni Amri Kiemba (Simba), Jonas Mkude (Simba) na Himid Mao kutoka Azam FC.
Washambuliaji ni Athanas Mdamu (Alliance Mwanza), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha (Azam), Ramadhan Singano (Simba) na Juma Luizio kutoka Mtibwa Sugar.

No comments:

Post a Comment