STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, March 5, 2014

Yanga kuivaa Alh Ahly J'2 usiku, kikosi kuondoka leo usiku

Kikosi cha Yanga kilichoibana Al Ahly kwa kuilaza 1-0 jijini Dar jumamosi iliyiopita
IMETHIBITIKA kuwa, wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika timu ya Young Africans itacheza mchezo wa marudiano siku ya jumapili jijini Cairo dhidi ya timu ya Al Ahly ukiwa ni mchezo utakaotoa picha halisi ni timu gani itasonga mbele katika hatua ya 16 bora.
Ikiwa ni takribani siku tano kabla ya kufanyika mchezo wenyewe wenyeji Al Ahly wameshindwa kuweka wazi ni uwanja gani utakaotumika kwa ajili ya mchezo huo huku Meneja wa klabu hiyo Abdoulazi akisema huenda mchezo ukachezwa jijini Cairo au Alexandria na kusema majibu kabili yatapatikana siku ya jumatano mchana.
Wenyeji wameiandalia timu ya Young Africans kufikia katika Hoteli ya Baron iliyopo maneneo ya Uwanja wa michezo wa kimataifa Cairo huku pia wakiipangia timu kufanya mazoezi katika uwanja wao uliopo eneno la Nasri City.
Katika mchezo wa awali uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Young Africans ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo shukrani kwa bao la Nahodha wa timu Nadir Haroub "Cannavaro" aliyetikisha nyavu dakika ya 82 ya mchezo.
Mara baada ya mchezo huo kikosi cha mholanzi Hans Van der Pluijm kiliingia kambini jana jioni katika hotel ya Ledger Bahari Beach tayari kwa maandalizi ya mchezo marudiano ambapo timu imeendelea kufanya mazoezi katika uwanja wa Boko Beach Veterani.
Kuelekea mchezo huo wa jumamosi tayari uongozi wa Young Africans ulishaanza kufanya maandalizi ya safari ambayo inatarajiwa kuwepo kabla ya mwisho mwa wiki hii huku msafara ukitarajiwa na kuwa idadi ya watu 35, wakimwemo viongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji 19.
Hali ya wachezaji ni nzuri, kiafya, fikra na morali ya kuelekea mchezo wenyewe bado ni kubwa kwani bench la ufundi na wachezaji wanaamini maandalizi wanayoyafanya yatasaidia kupelekea kupata ushindi katika mchezo huo na kuweza kusonga mbele katika hatua ya 16 bora.
Baadhi ya wachezaji wanaotarajiwa kuondoka usiku wa leo kuifuata Al Ahly ni makipa Deogratius Munishi 'Dida' na Juma Kaseja, Nadir Haroub 'Cannavaro, David Luhende, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Simon Msuva, Mrisho Ngasa, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbagu, Juma Abdul, Frank Domayo, Mbuyu Twite, Rajab Zahir na Said Bahanuzi.
Okwi na Kiiza, wataungana na kikosi hicho Alhamisi wakitokea Lusaka, walipo na timu yao ya Taifa ya Uganda ( The Cranes) ambayo jana ilikuwa inacheza na Zambia (Chipolopolo) mechi ya kimataifa ya kirafiki.
Yanga inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili iweze kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
Maandalizi ya sehemu ya kambi ambapo timu itafikia jijini Cairo tayari yanaendelea vizuri kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania ambapo kwa upande wa klabu ya Young Africans Afisa Habari Baraka Kizuguto tayari yupo nchini Misri kwa siku ya pili akiendelea kuweka mambo sawa.
Mchezo wa jumapili unatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Arab Contractors uliopo jijini Cairo huku mechi hiyo ikichezwa bila ya mashabiki kufuatia Serikali ya Misri kuzuia mashabiki wa soka kutokana na mashabiki hao kufanya vurugu katika mchezo wa Fainal ya Super Cup dhidi ya CS Sfaxien na kupelekea askari kadhaa kujeruhiwa.

No comments:

Post a Comment