STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, March 5, 2014

Wavuvi wawili wauwawa kwa risasi wakivua samaki mtoni

Na   Walter Mguluchuma, Katavi
WATU wawili  James  Mauto  21 Mkazi wa Kijiji  cha  Ugala Wilaya ya Mlele   na  January  Marekani  18 Mkazi wa Kijiji  cha Mtapenda  Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele  mkoa  wa Katavi wameuwawa  kwa kupigwa  risasi   na Askari wa Geme Reserve wakati  wakiwa wanavua  samaki  ndani ya   Hifadhi  ya Pori la akiba la Ugala na mwenzao mmoja kujeruhiwa  kwa Risasi sehemu ya mbavu zake
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa  wa Katavi Dhahiri Kidavashari   tukio hilolilitokea hapo  Februari  28 mwaka huu majira ya saa  tisa Alasiri  ndani ya Hifadhi ya pori  la akiba la Ugala Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi 

Alieleza siku hiyo ya tukio    James Mauti  na  Januari Marekani walikuwa wakivua samaki ndani ya mto Ugala uliko kwenye  Hifadhi  ya pori la akiba la ugala wakiwa na mwenzao mmoja  aitwaye  Seif Juma  40  Mkazi wa kijiji  cha Mtapenda  Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele
Kamanda Kidavashari alisema  wakati wakiwa wanaendelea kuvua samaki ndani ya mto huo  alitokea Askari  wa Geme Reserve  ambae alikuwa amevalia sare   huku akiwa na silaha  bunduki  ambayo haikuweza kufahamika aina yake
Alisema Askari huyo aliwaamuru  wavuvi  hao wajisalimishe kwake  hata hivyo wavuvi  hao waliokuwa wakiendelea na uvuvi  kufutia amri hiyo ya Askari  waliamua kutupa nyavu zao walizokuwa wakivulia samaki  na kukimbia mbio  kila mmoja sehemu yake
Ndipo Askari huyo  alipoanza  kuwarushia  risasi  wavuvi  hao  na kuwauwa  kwa risasi James Mauto   na Januari  Marekani  na kumjeruhi Seif  Juma sehemu za  mgongoni na kwenye mbavu
Majeruhi  ambae ni Seif  Juma  alifanikiwa  kufika katika kijiji  cha Ugala  na  kutoa taarifa kijijini hapo kwa uongozi wa Serikali ya Kijiji juu ya tukio hilo  na aliweza kupatiwa msaada wa kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya matibabu
Kamanda Kidashari  alieleza  kuwa mvuvi huyo  ambae ni majeruhi  kwa kuhofia kukamatwa na kuhojiwa  na polisi  baada ya kufikishwa  Hospitali alitoroka  na mpaka sasa  haijajulikana mahari alipo na anatibiwa wapi majeraha yake ya risasi
Alisema  kutokana na tukio hilo kuhusishwa  na Askari  wa Geme  Reserve  katika hifadhi  hiyo  jeshi la polisi Mkoa wa Katavi  linawasiliana  na mkuu wa  kikosi cha  wanyama pori  mkoa wa Tabora  ambako ndio  walikuwa wametoka Akari waliohusika na tukio la mauwaji hayo
Alifafanua  kuwa  tayari mkuu wa Kikosi hicho  cha wanyama pori  ametuma kikosi chake kwenye eneo hilo la tukio  ilikubaini  ni Askari  gani waliokuwa kwenye  doria  eneo hilo  ili kuwabaini  na kisha  sheria ichukuwe mkondo wake  kwa askari  aliyehusika au waliohusika  kwa tukio la mauwaji hayo ya kinyama kwa binadamu hao.
Pambana na Climate Change

No comments:

Post a Comment