STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, March 6, 2014

Taifa Stars angalau, yatoka sare ya 1-1 ugenini Namibia

Na Prince Akbar, Windhoek, Namibia
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imetoka sare ya kufungana bao 1-1 na Namibia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki unaotambuliwa na Fifa uliochezwa Jumatano usiku kwenye uwanja wa Sam Nujoma nchini Namibia.
Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika,timu hizo zilikuwa bado hazijafungana na kocha Salum Madadi akafanya mabadiliko katika kipindi cha pili kwa kuwatoa Erasto Nyoni, Ramadhani Singano ‘Messi’ na juma Luizio na nafasi zao kuchukuliwa na Michael Aidan, Athanas Mdam na khamisi Mcha ‘Vialli’.
Kikosi cha kwanza cha Timu ya Taifa, Taifa Stars kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Namibia, Brave Warriors na kutoka sare ya bao 1-1. Taifa Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Mchezaji wa Taifa Stars, Jonas Mkude  (katikati) akijaribu kupiga mpira katikati ya wachezaji wa timu ya taifa ya Namibia ‘Brave Warriors’ wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya timu hizo mbili katika uwanja wa Sam Nujoma  jana usiku. Tumu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Taifa Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Mlinzi wa Taifa Stars, Saidi Morad  (kulia) akiwania mpira na mchezaji wa timu ya taifa ya Namibia ‘Brave Warriors’ Lous Jereme  wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya timu hizo mbili katika uwanja wa Sam Nujoma jana usiku. Tumu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Taifa Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Mlinzi wa Taifa Stars, Erasto Nyoni (kulia) akijaribu kuudhibiti mpira mbele ya mchezaji wa timu ya taifa ya Namibia ‘Brave Warriors’ Puriza Hosea wakati wa mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya timu hizo mbili katika uwanja wa Sam Nujoma  jana usiku. Tumu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Taifa Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Stars, inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 86 baada ya kona  iliyopigwa na Khamisi Mcha ‘Vialli’ aliyetokea benchi na kuingia moja kwa moja nyavuni bila kuguswa.
Namibia walisawazisha bao hilo katika dakika ya tano ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za kawaida, lililofungwa na Nekundi Haleluya Panduleni kwa adhabu.
Refa wa mechi hiyo aliingia lawamani kwa kuzidisha muda kupita kiasi, kwani mwamuzi wa mezani alionyesha dakika tano za nyongeza lakini muamuzi alichezesha dakika tano nyingine hivi kuwawezesha Namibia kupata bao.
Lakini katika hali ya kushangaza waamuzi toka nchini Zambia na msimamizi wa mechi toka nchini Afrika Kusini waliopangiwa kuchezesha mchezo huo hawakutokea, na badala yake shirikisho la soka Namibia NFA, wakaamuru mchezo huo uchezeshwe na waamuzi wa Namibia kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Mwalimu Salum Madadi alisema licha ya kuwakosa wachezaji wengi nyota, kikosi hiki kilipigana hadi dakika ya mwisho na ameridhishwa na matokeo yaliyopatikana.
Wachezaji walioshindwa kujiunga na kikosi cha Stars ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mwinyi Kazimoto ambao hawakuruhusiwa na vilabu vyao kutokana na kukosekana na usafiri wa kuwarudisha vilabuni kwa muda unaotakiwa.
Wengine walioshindwa kufika ni Edward Charles na Hassan Masapili ambao hati zao za kusafiri hazikuwa zimekamilika. Viwango
Matokeo haya huenda yakaiweka Stars kwenye nafasi nzuri ya viwango vya Fifa kwa kupata sare ugenini.
BIN ZUBEIRY

No comments:

Post a Comment