STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, March 6, 2014

Cannavaro atamba Yanga itafanya maajabu Cairo

 
NAHODHA wa klabu ya Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema kwamba kikosi chao kitafanya maajabu kwenye mechi yao ya marudiano dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Klabu Bingwa Afrika, Al Ahly ya Misri siku ya Jumapili.
Yanga itaumana na Al Ahly katika mechi yao ya marudiano ya hatua ya kwanza itakayochezwa usiku wakiwa na ushindi wa 1-0 waliopata katika pambano lao la awali jijini Dar es Salaam kupitia goli lililofungwa kwa kichwa katika dakika ya 82 na nahodha huyo.
Akizungumza na MICHARAZO, Cannavaro alisema wanajua wa mchezo huo utakuwa ni mgumu, lakini wanaenda Cairo kuhakikisha wanatimiza ndoto zao za kuivusha Yanga kwenye 16 Bora.
"Tutaenda kupambana japo tunatarajia ushindani mkubwa baada ya kuwafunga hapa nyumbani," alisema beki huyo wa kati.
Cannavaro alisema wachezaji karibu wote watakaokuwa kwenye msafara wao uliotarajiwa kuondoka usiku wa jana, wamepania kuhakikisha Yanga inaing'oa Al Ahly na kurejea kilichowahi kufanywa na watani zao Simba mwaka 2003.
Katika mwaka huo Simba iliwafunga waliokuwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa, Zamalek pia ya Misri kisha kwenda kukubali kipigo cha 1-0 ugenini na kufanya timu hizo zikipigiane penalti na Simba kushinda kwa mikwaju 3-2.
"Tupo tayari kwa vita na Inshallah tutapambana mpaka kieleweke mjini Cairo kwa sababu tumepania kuifikisha mbali timu yetu, " alisema Cannavaro.
Bao la Cannavaro alililofungwa kwa kichwa cha kuchupia liliiwezesha Yanga kuvunja uteja kwa timu za Afrika Kaskazini zikiwamo kutoka Misri uliodumu kwa miaka zaidi ya 30 na watalazimika kupata japo sare ugenini ili kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment