STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, March 6, 2014

Yanga wapaa kuifuata Al Ahly ikijiamini

KIKOSI cha wachezaji 18 na viongozi wa klabu ya Yanga wameodnoka nchini usiku wa kuamkia leo kuelekea Misri kwa ajili ya pambano lao la marudiano dhidi ya Al Ahly wakijiamini wanaenda kumaliza kazi.

Msafara huo umeondoka bila nyota wake kutoka Uganda,Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi waliokuwa nchini Zambia kuichezea timu yao ya taifa Uganda The Cranes ambao walilala 2-1 kwa wenyeji wao Chipolopolo.
Hata hivyo wachezaji hao wanatarajiwa kuungana nao wenzao nchini Misri baadaye leo mchana wakitokea Zambia tayari kuivusha Yanga kwenye hatua ya 32 na kuipeleka katika 16 Bora mbele ya mabingwa wateteziu hao wa Ligi ya Mabingwa Afrika na mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo.
Wachezaji waliondoka kwenda kuiua Al Ahly ni  Ally Mustapha ‘Barthez’, Juma Kaseja, Deogratius Munishi ‘Dida’, Nadir Haroub ‘Cannavaro, Juma Abdul, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Oscar Jushua, Nizar Alfan, Franck Domayo, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Mrisho Ngasa, Said Bahanuzi, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbagu, David Luhende na Jerry Tegete.
Kwa mujibu wa uongozi wa Yanga mpaka sasa hawajajua mechi yao itakayochezwa Jumapili usiku itafanyika kwenye uwanja gani baada ya uongozi wa Al Ahly kuficha taarifa hizo mpaka jana mchana.
Hata hivyo, Afisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto aliyetangulia Cairo alsema huenda  mchezo huo ukachezwa kwenye Uwanja wa Arab Contractors uliopo jijini Cairo. na kwamba maandalizi ya kuipokea timu yao inaendelea vyema kujipanga kuivaa wenyeji wao ambao hawaamini mpaka sasa kama walefungwa na timu ya Afrika Mashariki .

No comments:

Post a Comment