STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 9, 2014

AFC Leopards yatupwa nje Kombe la Shirikisho Afrika

Orange CAF Confederation Cup: SuperSport vs AFC Leopards clash
AFC Leopards

KLABU kongwe ya Kenya, AFC Leopards jioni hii imeyaaga mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na Supersport ya Afrika Kusini.
Katika mechi hiyo ya marudiano iliyochezwa uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi Leopards imejikuta ikikwama kusonga mbele kwa Wasauzi baada ya wiki iliyopita kukubali kipigo cha mabao 2-0 ugenini na hivyo kung'olewa mashindanoni kwa jumla ya magoli 4-2.
Wenyeji walikuwa wa kwanza kupata bao maara baada ya kipindi cha pili kuanza baada ya kufanikiwa kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa nguvu sawa ya bila kufungana.
Bao hilo lilifungwa na dakika ya 48 kupitia James Situma, lakini wageni walisawazisha dakika ya 54 kupitia Thuso Phala kabla Supersport kuongeza la pili kupitia kwa Sameehg Doutie katika dakika ya 79 na kuwafanya Leopards kucharuka ili kuepuka kipigo cha nyumbani.
Juhudi hizo zilizaa matunda dakika ya 90 wakati Allan Wanga kulisawazisha bao hilo na kufanya matokeo kuwa 2-2, matokeo ambayo hata hivyo hayakuwasaidia Wabaluya kusonga mbele dhidi ya wageni.
Katika mchezo mwingine wa michuano hiyo Bizertin ya Tunisia nayo ilifuzu raundi ya pili baada ya kuinyuka Desportivo Huila ya Angola kwa mabao 2-0.
Watunisia walikuwa nyumbani na ushindi huo umeifanya kutinga raundi nyingine kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya wiki iliyopita kushinda 1-0 ugenini nchini Angola.

No comments:

Post a Comment