STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 9, 2014

Atletico Madrid yashinda ugenini na kuiporomosha Barca

Villa akipongezwa na wachezaji wenzake
MABAO mawili ya David Villa usiku wa kuamkia leo yaliiwezesha Atletico Madrid kurejea nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania na kuiporomosha Fc Barcelona hadi nafasi ya tatu baada ya kuinyuka  Celta Vigo ikiwa kwao kwa mabao 2-0.
Villa alifunga mabao hayo ndani ya dakika mbili dakika ya 62 na 64 na kuiwezesha timu yake iliyocheza bila 'muuaji' wake Diego Costa anayetumikia kadi nyekundu kufikisha p[ointi 64 kulingana na Real Madrid ambayo ina mchezo mmoja mkononi ambao itaucheza leo.
Timu hizo zinatofautiana uwiano wa mabao Madrid ikiizidi Atletico mabao matano tu na kuitangulia watetezi wa ligi hiyo Barcelona ambao jana walichezea kichapo cha bao 1-0 toka kwa Real Vallodolid kwa pointi moja kwani yenyewe ina pointi 63.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa leo  Jumapili, Grenada ilijipatia ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya wageniu wao Villarreal.
Kipute cha ligi hiyo kitaendelea tena leo kwa michezo kadhaa ambayo inaweza kuiongeza pengo la pointi baina ya vinara Real Madrid dhidi ya wapinzani wake waliopo ndani ya Tatu Bora.No comments:

Post a Comment