STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 9, 2014

Nusu Fainali FA ni Hull City vs Sheffield Utd, Arsenal vs Wigan (?)

USHINDI iliyopata jioni hii dhidi ya Sunderland imeifanya Hull City kukutana uso kwa uso na Sheffield United katika mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la FA, huku Arsenal wakisubiri mshindi kati ya Wigan Athletic inayoongoza mpaka sasa dhidi ya Manchester City katika hatua hiyo.
Kwa mujibu wa droo iliyotangazwa muda mfupi uliopita mechi za hatua hiyo zitacheza kati ya Aprili 12 na 13 kwenye uwanja wa Wembley jijini London.
Tumaini ya mashabiki wengi kutaka kuona nusu fainali ya aina yake kati ya Arsenal na Manchester City ni kama inapotea kwani mpaka sasa City wakiwa nyumbani wameshanyukwa mabao 2-1 na Wigan japo imesalia dakika 10 pambano hilo kumalizika, Samir Nasir alifunga bao la Man City baada ya muda mwingi Wigan kuongoza 2-0.
Iwapo City itashindwa kupenya hatua hiyo itafanya ndoto za kocha wa timu hiyo Manuel Pellegrini wa kuiwezesha timu hiyo kutwaa mataji manne msimu huu baada ya awali kunyakua Kombe la Ligi (Capital One) na Jumatano ana kibarua kigumu mbele ya Barcelona kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya awali kulala 2-0 nyumbani wiki mbili zilizopita.

No comments:

Post a Comment