STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, March 11, 2014

Arsenal kusuka au kunyoa kwa Bavarian

Arsenal watashangilia leo Ujeruman kama hivi kwa Bavarians
 ARSENAL yenye morali baada ya kufanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la FA, usiku huu itakuwa ugenini nchini Ujerumani kujaribu kupenya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bayern Munich.
Wakali hao wa London Kaskazini walitoka kuifumua Everton kwa mabao 4-1 katika mchezo wa Robo Fainali na leo itataka kuthibitisha kuwa msimu huu imepania angalau kuambuli mojawapo ya mataji ya ubingwa baada ya misimu karibu nane ikitoka patupu.
Ikiwa nyumba kwa mabao 2-0 ilipofumuliwa nyumbani na Bavarian, Arsenal itajarubuy kupambana na kuzika mzimu wa kutolewa kwenye 16 Bora kwa misimu karibu minne.
Msimu ulipita ni Bayern Munich iliyowakwamisha baada ya kuwatungua nyumbani kwao 3-1 kisha kupata ushindi Ujerumani kwa mabao 2-0 hata hivyo ikatoka kwa faida ya mabao ya ugenini, kitendo kilichomuudhi koca Arsene Wenger kiasi cha kulitaka Shirikisho la Ulaya, UEFA kuangalia upta sheria hiyo.
Arsenal imepewa nafasi kubwa ya kuitoa nishai Bayern kama ilivyofanya msimu uliopita, ila kazi ipo kwao kutokana na ubora na kiwango cha juu ilichonacho Bavarian kwa sasa, ikicheza mechi 16 na kufunga jumla ya mabao 26.
Wikiendi hii wakati Arsenal ikiigaragaza Everton, wenyewe waliichachafya  VfL Wolfsburg kwa mabao 6-1 ingawa kocha wake, Pep Guardiola amenukuliwa akiwahofia wapinzani wao na hasa kama wachezaji waop wataamua kuwaacha wamiliki mpira.
Kurejea katika kiwango kwa Mesut Ozil na majeruhi kadhaa katika kikosi cha Gunners kunawapa matumaioni makubwa mashabiki wa Arsenal kwamba leo watavunja mwiko wa kuishia 16t Bora kwa misimu minne mfululizo kwa kuing'oa Bayern Munich na kuivua taji la michuano hiyo.
Hata hivyuo Bayern wapo vyema na hasa baada ya kurejea kwa nyota wao, Frank Ribery aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu kumeiongezea chachu ya kuhakikisha wanatinga robo fainali na kuendeela kujipa matumaini ya kutetea taji hilo.
Mbali na mechi hiyo pia leo kuna mechi nyingine ambayo inaikutanishaAtletico Madrid itakayokuwa nyumbani kurejea na AC Milan ambayo walikubali kipigo nyumbani kwao katika mechi iliyopita ya kwanza.
Michezo mingine inatarajiwa kuchezwa kesho kwa pambano la kukata na mundu kati ya Barcelona itakayokuwa nyumbani kuikaribisha Manchester City waliotota katika mechi ya kwanza kwa mabao 2-0 na pia wikiendi hii kujikuta wakitupwa nje kwenye michuano ya FA baada ya kuzabuliwa na watetezi wa taji hilo, Wigan Athletic kwa mabao 2-1.
Pia kesho PSG iliyopata ushindi mnono wa mabao 4-0 ugenini itaialika Bayer Leverkusen mjini Paris ili kuhitimisha nafasi yake ya kutinga robo fainali.

No comments:

Post a Comment