STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 24, 2015

Nahodha wa Gabon akiri kuchemsha kwa Congo

http://www.africatopsports.com/wp-content/uploads/2014/12/aubagabon.jpg
Pierre Emerick Aubameyang
MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya taifa ya Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang amekiri kuwa chini ya kiwango katika mchezo waliofugwa dhidi ya Congo Brazzaville ambao timu yake ililazwa bao 1-0.
Baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Burkina Faso katika mchezo wao wa ufunguzi Jumamosi iliyopita, Gabon walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda katika mchezo huo lakini mambo yalibadilika baada ya Congo kuwafunga bao 1-0.
Aubemeyang ambaye alikuwa nyota katika mchezo wao wa kwanza amekiri kuwa hakuwa katika kiwango chake katika mchezo dhidi ya Congo.
Nyota huyo anayekipiga katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani amesema walishindwa kutengeza na kutumia mchezo wao hali ambayo iliwafanya kuiga mchezo wa wapinzani jambo lililokuwa baya kwao. Hata hivyo, Aubameyang anaamini wanaweza kuamka katika mchezo wa mwisho na kuhakikisha wanaibuka na ushindi.
Timu hiyo itashuka dimbani kesho dhidi ya wenyeji Guinea ya Ikweta katika pambano la kuamua timu zipi za kutinga robo fainali za zipi za kurudi makwao.
Katika kundi hilo Congo wanaongoza msimamo wakiwa na pointi nne wakifuatiwa na Gabon, kisha Guinea ya Ikweta yenye pointi 2 na inayoburuza mkia ni Burkina Faso yenye pointi moja.

No comments:

Post a Comment