STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 24, 2015

Algeria yagongwa, Afrika Kusini huzuni, Mali, Ivory Coast kivumbi leo

Senegal's defender Kara Mbodji (right) celebrates after scoring the equaliser against South Africa
Kara Mbodji akishangilia bao la kusawazisha la Senegal dhidi ya Afrika Kusini
Gyan celebrates, while team-mate - Crystal Palace youngster Kwesi Appiah - is seen behind
Asamoah akishangilia bao pekee la Ghana dhidi ya Algeria
Tempers flared between Ghana and Algeria during the Africa Cup of Nations Group C match in Mongomo
Ubabe mtupu kati ya Algeria na Ghana
WAKATI timu ya Afrika Kusini ikijiweka katika mazingira magumu ya kusonga mbele kwenye kundi C la michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Ghana wenyewe wamezinduka na kuidunga 'vijogoo' wa Afrika, Algeria kwa kuichapa bao moja katika mechi za raundi ya pili ya kundi hilo.
Bafana Bafana walishindwa kulinda bao lao dhidi ya Senegal katika mechi iliyochezwa usiku wa jana na kuambulia pointi moja ikiwaacha wakiwa mkiani mwa msimamo wa kundi hilo la 'kifo'.
Afrika Kusini walioanza vibaya michuano hiyo kwa kufungwa mabao 3-1 na Algeria, walitangulia kupata bao dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza kupitia kwa Oupa Manyisa kabla ya Senegal walioilaza Ghana kwenye mchezo wao wa kwanza kusawazisha dakika ya 60 kupitia kwa Kara Mbodji.
Sare hiyo imeiweka Senegal kileleni mwa kundi hilo wakiwa na pointi nne wakifuatiwa na Algeria ambayo ilicharazwa bao 1-0 na Ghana iliyopo nafasi ya tatu kwa bao la dakika za jioni lililowekwa kimiani na nahodha wa Black Stars, Asamoah Gyan.
Kivumbi cha michuano hiyo kuhitimisha raundi ya pili kitaendelea leo kwa michezo ya kundi D ambapo Mali watavaana na Ivory Coast kabla ya Cameroon kujiuliza kwa Guinea. Timu zote nne katika mechi zao za awali waliambulia sare ya 1-1 na hivyo kulingana kwa kila kitu katika kundi hilo.

No comments:

Post a Comment