STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 24, 2015

Yanga vitani na Polisi Moro, Simba, Azam hapatoshi Taifa

Yanga kuendeleza sare au kuvunja mwiko Jamhuri
Polisi Moro kuvuna nini kwa Yanga leo?
Simba wataendeleza ubabe wao mbele ya Azam
Azam watakaojiuliza kwa Simba kesho Taifa

Mtibwa Sugar watakuwa wageni wa Ruvu Shooting
Ndanda Fc watakaokuwa ugenini dhidi ya Kagera Sugar
BAADA ya kulazimishwa sare mbili mfululizo kiasi cha kuanza kupagawa, Yanga leo watakuwa uwanja wa ugenini Jamhuri, Morogoro kupambana na Polisi Moro katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga imekuwa na bahati mbaya na uwanja wa Jamhuri, hivyo pambano lao la leo watahitajika kupigana kiume ili kupata ushindi na pia kujiweka katika nafasi nzuri ya kuufukuzia ubingwa unaoshikiliwa na Azam ambao wapo kileleni mwa msimamo na watakaokuwa na kibarua kizito kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar kuvaana na Simba.
Yanga waliopo nafasi ya nne kwenye msimamo wakilingana pointi sawa na Polisi Moro, hawajaonja ushindi wowote tangu ligi itoke mapumziko.
Timu hiyo inayonolewa na kocha Hans van der Pluijm na Charles Boniface Mkwasa waliorejeshwa baada ya aliyekuwa kocha wao, Marcio Maximo kutimuliwa baada ya ligi kusimama Novemba 9, ilianza mechi zake kwa kupata sare ya 2-2 na Azam kabla ya kuambulia 0-0 katika mechi iliyojaa ubabe.
Kocha Pluijm atakuwa na kazi kubwa ya kuwazuia vijana wa nyota wa zamani wa kimataifa wa Tanzania aliyetamba na timu za Yanga na Pan Africans, Mohammed Rishard 'Adolph' kutokana na ukweli Polisi waliorejea ligi kuu msimu huu wapo vema.
Yanga itashuka dimbani bila huduma za baadhi ya nyota wake ambao ni majeruhi akiwamo beki kiraka Mbuyi Twite.
Kivumbi cha ligi hiyo kitaendelea pia leo kwenye uwanja wa Mabatini kwa mchezo kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Mtibwa Sugar, kabla ya kesho kushuhudiwa michezo kadhaa likiwamo la Azam na Simba ambazo zitaumna kwenye uwanja wa Taifa.
Simba walioshinda mechi zao mbili mfululizo wakitokea kunyakua Kombe la Mapinduzi, wameapa kuwatoa nishai Azam ambao wametoka kupata ushindi katika mechi mbili za ugenini dhidi ya Stand United na Kagera Sugar.
mechi nyingine za kesho zitakutanisha mahasimu wa jadi wa jijini Mbeya, Prisons dhidi ya Mbeya City mechi itakayochezwa uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Pia Kagera Sugar watakuwa nyumbani uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kuumana na Ndanda ya Mtwara, huku Stand itaialika Coastal Union uwanja wa Kambarage Shinyanga na Mgambo JKT itakuwa wageni wa JKT Ruvu pambano litakalochezwa uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam.
Mpaka sasa msimamo unaaoonyesha Azam wanaongoza msimamo wakiwa na pointi 20 kutokana na mechi 10 wakifuatiwa na Mtibwa Sugar wenye pointi 17 kisha JKT Ruvu wenye pointi sawa na Mtibwa na kufautiwa na Yanga yenye pointi 15 sawa na Polisi Moro wanaowafuata nyuma yao.
Msimamo kamili wa Ligi hiyo mpaka sasa ni kama ifuatavyo;









1
Azam 106 2 2 147 20
2
Mtibwa Sugar 9 4 5 0 127 17
3
JKT Ruvu 11 5 2 4 111 17
4
Young Africans 9 4 3 2 114 15
5
Polisi Morogoro 11 3 6 2 91 15
6
Kagera Sugar 11 3 5 3 80 14
7
Coastal Union 10 3 4 3 91 13
8
Mgambo JKT 10 4 1 5 5-4 13
9
Simba 9 2 6 1 92 12
10
Ruvu Shooting 11 3 3 5 5-3 12
11
Mbeya City 9 3 2 4 4-2 11
12
Stand United 11 2 5 4 7-6 11
13
Ndanda 11 3 1 7 10-6 10
14
Prisons 10 1 5 4 6-2 8

No comments:

Post a Comment