STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, September 4, 2014

Lahm, Klose watunukiwa Ujerumani ikilala 4-2 kwa Argentina

http://content4.promiflash.de/article-images/w500/philipp-lahm-per-mertesacker-und-miroslav-klose-werden-aus-dfb-team-verabschiedet.jpg 04 Sep 2014 BAADA ya kazi nzuri waliyoifanyia nchi ya Ujerumani, wachezaji wakongwe Miloslav Klose, Philipp Lahm na Per Mertesacker wamepewa tuzo za heshima jana kabla ya mchezo wa kirafiki kati ya Ujerumani na Argentina Uwanja wa Esprit Arena ambao ulishuhudiwa Ujerumani ikinyukwa mabao 4-2.
Watatu hao waliichezea Ujerumani katika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014 dhidi ya Argentina kabla ya kuamua kustaafu soka ya kimataifa.
Klose, ambaye ni mfungaji bora wa kihistoria wa Ujerumani kwa mabao yake 71, ametungika daluga baada ya kuwa mfungaji wa mabao mengi zaidi katika historia ya Kombe la Dunia.
Hata hivyo furaha yao ya kupokea tuzo hizo ziliingia shubiri baada ya kuishuhudia Ujerumani ikifa mbele ya Argentina.
Winga mpya wa Manchester United,  Angel di Maria ametengeneza mabao matatu na kufunga moja katika mchezo huo uliochezwa mjini Dusseldorf, Ujerumani.
Mchezaji huyo ghali zaidi kusajiliwa Manchester United na Uingereza nzima alipika mabao ya Sergio Aguero, Erik Lamela na Federico Fernandez kabla ya kufunga na lake mwenyewe siku 52 tangu bao la Mario Gotze katika muda wa nyongeza liipe Ujerumani ubingwa wa dunia nchini Brazil. 
Ujerumani walipata mabao yao kupitia Andre Schurrle Gotze aliyefunga la pili kwa mabingwa hao wa dunia.

No comments:

Post a Comment