STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 7, 2014

Esha Buheti achekelea tuzo mbili kwa mpigo

Esha Buheti akiwa na tuzo yake ya ACVCA-2014
http://2.bp.blogspot.com/-RLZp_l7brig/VBFh6i_4LAI/AAAAAAAANMA/d5c-rUNNvmE/s1600/2.jpg
Esha Buheti katika pozi
MSHINDI wa Tuzo za filamu za Action & Cuts Viewers Choice (ACVCA-2014) Esha Buheti amesema mafanikio aliyopata kwa kipindi kifupi katika tasnia hiyo imetokana na kipaji cha kuzaliwa, kujituma na kujiheshimu mbele ya jamii.
Esha alisema, amejisikia faraja kuona ndani ya kipindi kisichozidi miezi mitatu akinyakua tuzo ya pili baada ya ile ya ZIFF-2014 (Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar) na katu hatavimba kichwa badala yake kuongeza bidii afike mbali zaidi.
Mrembo huyo alisema kuwashinda nyota wa filamu kama Chuchu Hans, Salma Jabu 'Nisha', Shamsa Ford na Blandina Chagula 'Johari' siyo kazi ndogo na kusisitiza anashukuru wote waliopigia kura za kutosha na kunyakua tuzo hiyo ya pili.
"Kwa kweli nimejisikia faraja kubwa kwa lililonitokea, sikuamini kama ningeweza kuibukia mshindi mbele ya washindani wangu ambao naamini ni wakali. Hii ni changamoto kwangu kundelea kufanya vyema ili nitambe kimataifa," alisema.
Muigizaji huyo alishinda tuzo hiyo wiki iliyopita katika kipengele cha Muigizaji Bora Msaidizi, ikiwa ni miezi mitatu tangu alipotwaa tuo ya Muigizaji Bora wa Kike wa ZIFF-2014 kupitia filamu ya 'Mimi na Mungu Wangu' anayoitaja kama kazi bomba kwake.

No comments:

Post a Comment