Kama wanavyopeana sapoti kwenye tuzo wasanii wanapaswa pia kuhudhuria semina mbalimbali kupata uelewa na wa mambo yanayowakwaza |
Na Kipimo Abdallah
UMOJA wa Mashirikisho ya Sanaa Tanzania umewaomba
wasanii nchini kujitokeza katika semina ambayo inatarajia kufanyaka Oktoba
mwaka huu katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Umoja huo
Godfrey Ndimbo wakati akizunumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam.
Alisema umoja wao unatoa pongezi kwa taasisi hiyo ya
Haki Neel Production Company ambayo imetambua msanii wa Tanzania.
Ndimbo alisema semina hiyo itajikita katika
kuwaelimisha wasanii kuhusu mafao ya uzeeni, matibabu kupitia bima ya afya,
Haki Miliki, Haki Shiriki na Kodi.
“Napenda kuwaomba wasanii wa Tanzania kujitokeza kwa
wingi katika semina hiyo kwani itawajengea uwezo mzuri katika kutambua haki zao
nyingi ambazo zinakiukwa, ” alisema.
Ndimbo alisema katika semina hiyo wanatarajia
kuwahusisha watumishi kutoka taasisi mbalimbali kama Poilisi, Uhamiaji na Mahakimu.
Katibu Mkuu huyo alisema lengo la kushirikisha sekta
hizo ni kuhakikisha kuwa wanakuwa na ufahamu dhidi ya kazi hizo za wasanii
nchini ili wajione kuwa wana haki ya kutetea kazi hizo.
Alisema lengo ni kuhakikisha kuwa sheria inayotumika
kutoa hukumu kwa husika inakuwa na tija kwani kwa sasa ni ndogo jambo ambalo
linakwamisha maendele ya tasnia hiyo.
Katibu Mkuu huyo alisema pia wanawakaribisha
waandishi wa habari katika semina hiyo ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na ufahamu
mzuri wa kutosha kuhusiana na tasnia hiyo.
Alitoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kwa wingi
ili kusaidia na taasisi ya Haak Neel Production Company ambayo imeonyesha
jitihada za kutambua nafasi ya msanii.
mwisho
No comments:
Post a Comment