Yanga wanaenda mapumziko wakipumua nafasi ya tatu |
Coastal Union bado wanajikongoja |
Watetezi Azam wakiporomoka hadi nafasi ya pili wakiwapisha Mtibwa kuwaongoza |
Mtibwa timu pekee iliyoshinda mechi zake 100% |
Ruvu Shooting ndiyo ambayo haijafunga bao hata mmoja mpaka sasa. Ni kwamba pengo la Maguli (kushoto) halijapata mrithi wa kuliziba? |
Simba wataivaa Yanga mechi ijayo ikiandamwa na mdudu wa sare |
Kavumbagu aliyetua Azam akitokea Azam anafuatiwa kwa karibuni na Ally Shomari wa Mtibwa mwenye mabao matatu kiisha kufuatiwa na wachezaji wanne wenye mabao mawili kila mmoja.
Timu yenye fowadi kali mpaka sasa wakati lihi ikienda mapumziko kwa wiki moja ni Mtibwa Sugar na Ndanda FC zenye mabao sita kila moja, kisha kufuatiwa na Azam yenye mabao matano kisha Yanga na Simba zikafuatia zikiwa zimetumbukiza kimiani mabao manne kila moja.
Pamoja na kuwa kinara wa kufunga mabao Ndanda pia ndiyo timu yenye ukuta mwepesi ikiruhusu mabao sita mpaka sasa ikifuatiwa na timu za Stanmd United na Polisi waliopanda pamoja ligi ya msimu huu zikiwa zimeruhusu mabao matano.
Ruvu Shooting ndiyo timu iliyo na safu butu mpaka sasa ikiwa haijafunga bao lolotewakifuatiwa na Mbeya City, Mgambo na JKT Ruvu wenye bao moja moja.
Ukuta wa chuma wa ligi hiyo mpaka sasa ni ule wa klabu ya Mbeya City ambayo haujaruhusu bao lolote kwake huku Mtibwa Sugar na Azam zikifuata kwa kufungwa bao moja tu kila moja.
Yanga ambayo ilianza kwa kipigo katika ligi ya msimu huu imechupa toka maeneo ya kati hadi nafasi ya tatu wakiwaacha watani zao watakaoumana nao katika mechi yao ijayo wakiwa na pointi tatu wakishika nafasi ya 10.
MSIMAMO KAMILI WA LIGI KUU TANZANIA BARA 2014-2015
P W D L F A GD Pts
01. Mtibwa Sugar 03 03 00 00 06 01 +5 09
02. Azam 03 02 01 00 05 01 +4 07
03.Yanga 03 02 00 01 04 04 00 06
04. Mbeya City 03 01 02 00 01 00 +1 05
05.Kagera Sugar 03 01 01 01 03 02 +1 04
06. Prisons 03 01 01 01 03 02 +1 04
07.Coastal Union 03 01 01 01 04 04 00 04
08.Stand Utd 03 01 01 01 03 05 -2 04
09. Ndanda Fc 03 01 00 02 06 06 00 03
10.Simba 03 00 03 00 04 04 00 03
11. Mgambo JKT 03 01 00 02 01 02 -1 03
12. Polisi Moro 03 00 02 01 03 05 -2 02
13.JKT Ruvu 03 00 01 02 01 04 -3 01
14. Ruvu Shooting 03 00 01 02 00 04 -4 01
Didier Kavumbangu (kushoto) akipongezwa na wenzake |
4- Didier Kavumbagu(Azam)
3- Ally Shomari (Mtibwa)
2- Shaaban Kisiga (Simba), Nassor Kapama (Ndanda), Ame Ally (Mtibwa), Rashind Mandawa (Kagera)
1- Emmanuel Okwi, Amissi Tambwe (Simba), Coutinho, Kelvin Yondan, Haruna Niyonzima, Simon Msuva (Yanga), Deo Julius (Mbeya City), Danny Mrwanda, Nicolaus Kabipe, Bakari (Polisi-Moro), Salum Kanoni, (Kagera), Aggrey Morris (Azam), Ernest Joseph, Paul Ngalema, (Ndanda), Jacob Mwaitalako, Ibrahim Kihaka, Laurian Mpalile (Prisons), Lutimba Yayo, Rama Salimu, Joseph Mahundi, Hussein Sued, (Coastal), Ramadhani Pella (Mgambo), Mussa Mgosi (Mtibwa), Jabir Aziz (JKT Ruvu), Salum Kamana, Heri Mohammed, Mussa Said(Stand Utd)
No comments:
Post a Comment