STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 7, 2014

SHIWATA kuadhimisha Miaka 10 kwa sherehe la nguvu

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Twalib 'Teacher' akifafanua jambo kwenye mkutano na wanahabari hivi karibuni
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (Shiwata) wenye maskani yake Ilala jijini Dar es Salaam, unatarajia kufanya sherehe ya kutimiza miaka kumi tangu ulipoanzishwa Desemba mwaka 2004.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa mtandao huo, Cassim Talib, sherehe hizo zitafanyika Desemba mwaka huu katika kijiji cha wasanii kilichopo Mwanzega wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Talib alisema kuwa katika sherehe hizo ambazo zitapambwa na burudani za mpira wa miguu, ngumi, ngoma za asili na nyingine nyingi kutoka kwa wasanii ambao ni wanachama wa Shiwata.
"Katika sherehe yetu hiyo ya kutimiza miaka kumi tangu tulipoanzisha mtandao huu kutakuwa na zoezi la kugawa nyumba kwa wasanii ambazo zitakuwa zimekamilika wakati huo wa Desemba," alisema Talib.
Alisema kuwa mtandao huo una wanachama 8,000 ambao baadhi yao wamekuwa wakichangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za wasanii na sasa Shiwata imegawa 66 ambazo tayari zimekamilika..
Mwenyekiti huyo alisema kuwa kuna nyumba 45 ambazo zinaendelea kujengwa hadi sasa na kwamba ana uhakika kufikia Desemba zitakuwa zimekamilika na kugawiwa kwa wahusika wakati huo wa sherehe za kutimiza miaka kumi.
 "Tunatarajia kusherekea miaka kumi ya kuanishwa kwa mtandao wetu tukiwa tumepitia changamoto nyingi zikiwamo za kuzushiwa kuwa sisi ni matapeli na kila aina ya uzushi, lakini tumeshinda hizo njama za kutuhujumu na sasa tunaendelea kusonga mbele," alisema.

No comments:

Post a Comment