STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 9, 2016

Maskini Agger! Aamua kutundika daluga bila kupenda

http://i1.manchestereveningnews.co.uk/incoming/article660491.ece/ALTERNATES/s615/C_71_article_1584808_image_list_image_list_item_0_image.jpgHANA namna. Maumivu ambayo yamekuwa yakimuandama mara kwa mara nyota wa zamani wa Liverpool, Daniel Agger yamemfanya atundike daluga. Agger ametangaza kustaafu soka akiwa  ndio kwanza ana umri wa miaka 31 tu. Beki huyo amekuwa akisumbuliwa kwa kipindi kirefu cha soka lake la majeruhi aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuelezea uamuzi wake huo. Agger aliandika katika twitter akiwashukuru wale wote waliomuunga mkono katika kipindi chote na kuongeza japo ni uamuzi mgumu, lakini anadhani ni sahihi kwa afya yake.
Beki huyo wa kimataifa wa Denmark aliyeondoka Liverpool mwaka 2014 baada ya kuitumikia kwa miaka nane na kurejea katika klabu yake ya utotoni ya Brondby, amewahi kuichezea nchi hiyo mechi 75. Mkali huyo ameingia katika orodha ya nyota waliowahi kustaafu soka mapema kabla ya wakati wao kwa sababu mbalimbali ikiwamo majeruhi yasiyoisha.

No comments:

Post a Comment