STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 9, 2016

Real Madrid yawinda rekodi mpya kwa Pogba

http://static.independent.co.uk/s3fs-public/thumbnails/image/2015/08/25/20/pg-64-pogba-1-getty.jpg
Paul Pogba anayeingia rada za Real Madrid
MWENDO wa noti tu. Klabu ya Real Madrid ipo tayari kumwaga mkwanja wa nguvu ili kuipiku Manchester United inayotaka kumrejesha kikosini, Paul Pogba anayekipiga Juventus.
Klabu hiyo imedaiwa ipo tayari kutoa Pauni Milioni 94 ili kunasa saini ya Pobga anayewindwa na klabu yake ya zamani Man United walio tayari kuvunja benki na kumwaga Pauni Milioni 78.
Kwa mujibu wa gazeti maarufu la michezo la Gazzetta dello Sport la Italia limesema kuwa, Real Madrid imepania kumnasa kiungo huyo fundi kutoka Ufaransa, licha ya kwamba katika mbio hizo pia Matajiri wa Manchester City wapinzani wakuu wa Man United nao wanammendea kimyakimya.
Iwapo Rela itafanikiwa kumnasa Pogba kwa kiwango hicho cha fedha itakuwa imevunja rekodi inayoshikilia kwa sasa ya kumnasa Gareth Bale misimu mizili iliyopita ilipomwaga kiasi cha Pauni Milioni 80.
Gazeti hilo limefichua kuwa, Mkurugenzi wa Juventus Giuseppe 'Beppe' Marotta wiki ijayo anatarajiwa kutua Hisapnia kwa ajili ya mazungumzo ya uhamisho wa Alvaro Morata, lakini pia suala la Pobga litagusiwa.
Mashetani Wekundu pia walikuwa wakimnyatia Moratta, lakini inaonekana wazi Jose Mourinho atachemsha mbele ya mabosi wake wa zamani Real Madrid.

http://img.kiosko.net/2016/06/09/it/gazzetta_sport.750.jpg
gazeti lililodokeza mipango ya Real kutaka kuvunja rekodi ya kumnyakua Pogba

No comments:

Post a Comment