STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, June 9, 2016

Paul Pogba awaota kina Pele, Diego Euro 2016 watamkoma!

http://bolavip.cdnfsn.com/img/rankings/x/n1406834042.jpg
Paul Pogba
MBONA mtamkoma. Kiungo nyota wa Juventus aliyewahi kukipiga kwa Mashetani Wekundu, Manchester United, Paul Pogba amefunguka kwa kudai kuwa anataka akumbukwe kwa soka lake kama ilivyokuwa kwa kina Diego Maradona wa Argentina na Pele wa Brazil.
Pogba ambaye atakuwa na jukumu la kuisaidia nchi yake kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya (Uefa Euro 2016) inayofanyika kwao Ufaransa, alisema kuwa,  amepania kufikia malengo yake hayo kwa kujituma na kuhakikisha kila siku anaimarika.
Kiungo huyo aliyeiwezesha Juventus kunyakua mataji manne ya Ligi Kuu ya Serie A na kucheza fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka jana, amekuwa akizidi kuimarika na kuwa mmoja ya nyota wanaomezewa mate kwa ubora wake wa soka.
Pogba aliondoka United kuelekea kwa Kibibi Kizee cha Turin mwaka 2012 na akihojiwa na runinga ya ESPN, Pogba alisema  kwasasa hadhani kama ameshafanya lolote la maana katika soka kwa vile bado kuna mataji mengi hajawahi kushinda ikiwamo Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Dunia na hata Euro.
Hivyo amesema kuwa atapambana kiume katika ushiriki wake wa soka ili kuona anafika kule ambako kina Diego na Pele walifikia kiasi cha kubaki kuwa gumzo licha ya kustaafu kitambo na kuibuka kwa nyota mbalimbali duniani kwa sasa.

No comments:

Post a Comment