Bestina Magutu (kushoto) |
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA imetumia dola 310,000 sawa na shilingi milioni 496 kwa ajili ya kuwalipia ada wanafunzi watano ambao wanasomea urubani wa ndege nchini Afrika Kusini.
Hayo yamebainishwa na Afisa habari wa TCAA Bestina Magutu wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam.
Alisema wanafunzi hao wamepatikana baada ya mchujo wa wanafunzi 270 ambao waliomba ambapo walibakia 11 na baadae ndio wakapatikana hao awatano ambao wanalipiwa na TCAA.
Magutu alisema ufadhili ni kwa kila mwanafunzi kupatiwa dola 62,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 99 za Kitanzania ambapo watasoma kwa miezi 14 na mwishoni mwa mwa huu watakuwa wanahitimu.
Alisema jitihada za TCAA ni kuhakikisha kuwa idadi ya marubani inaongezeka kila mwaka ukizingatia kuwa wapo ambao wanastaafu na wengine wakifariki hivyo bu wajibu wa mamlaka hiyo kuongeza watu wa tasnia hiyo.
“TCAA tunajitahidi kuwapatia ufadhili wanafunzi ambao wanakuwa na sifa za kusoma urubani ambapo kwa sasa wapo watano wako Afrika Kusini ila gaharama ni kubwa hivyo tunaomba wadau kujitokeza kufanikisha zoezi hilo”, alisema Magutu.
Afisa Habari huyo wa TCAA alisema hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu idadi yamarubani ilikuwa 562 idadi ambayo ni ndogo kutokana na ukweli kuwa kumekuwepo kwa ongezeko kubwa la uwekezaji katika sekta hiyo.
Magutu alisema iwapo Serikali itaachiwa yenyewe katika kutoa mafunzo ya urubani ni wazi kuwa idadi itakuwa ndogo hali ambayo itachangia kazi nyingi kuchukuliwa na watu kutoka nje.
Alitoa wito kwa jamii kushirikiana ili kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na idadi kubwa ya watu wenye fani ya urubani ili kuhakikisha kuwa fursa zinazojitokeza wanaziitumia ipasavyo.
Aidha akizungumzia ni kwa nini wanafunzi hao wanaenda kusoma nje ya nchi na sio hapa nchini Ispecta Mwandamizi wa Idara ya Udhibiti Masuala ya Usalama wa Ndege Redemptus Bugomola alisema vyuo vilivyopo hapa nchini vinatoa elimu ya urushaji ndege za watu binafsi jambo ambalo haliwezi kukidhi hitaji la ndege za kibiashara na zile kubwa.
Bugomole alisema sekta anga ni moja ya sekta ambayo inahitaji uwepo wa watu wenye nia madhubuti ya kusoma kutokana na ukweli kuwa matumizi yake yanhitaji umakini wa hali ya juu.
No comments:
Post a Comment