STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, January 7, 2016

Rafa Benitez hana kinyogo na Real Madrid

http://img.thesun.co.uk/aidemitlum/archive/01682/SNF0108A---_1682580a.jpg
Kocha Rafa Benitez
LICHA ya kumtimua kazi, Meneja wa zamani wa Real Madrid, Rafael Benitez ametoa ya moyoni kwa kuishukuru klabu hiyo kwa kumpa nafasi na kumtakia kila la kheri mrithi wake Zinedine Zidane. 
Benitez alitimuliwa Jumatatu  ikiwa ni miezi sba tu tangu alipokabidhiwa timu hiyo na nafasi yake kuchukua nguli wa klabu hiyo Zidane ambaye alikuwa akikinoa kikosi B cha Castilla. 
Kuanza kampeni za msimu huu kwa kusuasua kikiwemo na kipigo cha mabao 4-0 kutoka mahasimu wao Barcelona kulichangia kwa kiasi kikubwa kutimuliwa kwa Benitez, huku mgomo baridi katika vyumba vya kubadilishia nguo nao ukitajwa kuchangia pia. 
Lakini katika taarifa yake aliyotoa katika matandao wake, Benitez amewahakikishia kuwa hana kinyongo chochote kufuatia kutimuliwa kwake.  
Kocha huyo amesema imekuwa ni heshima kubwa kwake kupata nafasi ya kuinoa klabu hiyo hivyo anawashukuru viongozi, wafanyakazi, wachezaji na mashabiki kwa kumuunga kwao mkono katika kipindi chote alichokuwepo Santiago Bernabeu.
Chini ya Benitez, Real Madrid ilishindwa kupata ushindi katika mechi nane, saba zikiwa za La Liga na moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na sare ya 2-2 dhidi ya Valencia ilikuwa tiketi yake ya kutimuliwa klabuni hapo.

No comments:

Post a Comment