STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, January 7, 2016

Tanzania yapanda nafasi 6 Fifa, Uganda noma!

Wachezaji wa Taifa Stars katika moja ya mechi zao za kimataifa
TANZANIA imepanda kwa nafasi sita kwenye msimamo wa Orodha ya Viwango vya Soka vya Dunia, ikishika nafasi ya 126 kutoka ile ya 132 iliyoshikilia Desemba mwaka jana.
Kwa mujibu wa orodha mpya iliyotolewa leo Alhamisi, Uganda imeweka rekodi ya kushika nafasi ya 62 ikiwa nafasi ya juu zaidi kuwahi kushikwa na taifa hilo la Afrika Mashariki ikipanda nafasi moja juu. Desemba ilikuwa nafasi ya 63, huku Rwanda, Kenya, Burundi na Ethiopia zikiifuata nchi hiyo katika orodha hiyo kwa nchi za ukanda huo wa Afrika Mashariki.
Ivory Coast, Algeria zimeendelea kukomaa kwenye nafasi zao mbili za juu sawa na ilivyo kwa Ghana na Cape Verde kwa upande wa Afrika zikishika nafasi ya 19, 28, 33 na 39 duniani, huku Ubelgiji anapotaka kwenda kucheza soka la kulipwa nyota wa Afrika na Tanzania, Mbwana Samatta ikiendelea kuongoza orodha hiyo ya ubora dunia wakifuatiwa na Argentina, Hispania na Ujerumani katika nafasi nne Bora.

Top 10 ya Dunia:

1. Ubelgiji
2. Argentina
3 Hispania
4. Ujerumani
5. Chile
6. Brazili
7.Ureno
8. Colombia
9.England
10. Austria

Top 10 ya Afrika:

1. Ivory Coast
2. Algeria
3. Ghana
4. Cape Verde
5. Tunisia
6. Senegal
7. Congo
8. Guinea
9. Cameroon
10. Misri

Top 10 ya Cecafa:

1. Uganda
2. Rwanda
3. Kenya
4. Burundi
5. Ethiopia
6. Tanzania
7. Sudan
8. Sudan Kusini
9. Djibout
10. Eritrea

No comments:

Post a Comment