STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, August 22, 2015

PATACHIMBIKA TAIFA, YANGA v AZAM NI SHEEDA!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjpjkGwXmOK250PzIJkj4gA7pkZ1mMpkKFXP2MG3mX3y_l3IHb7aHldzJdHcS2u-VTXyZldrrwgZtbd-yV0ndewKQDYjerOJ3aSNEVPxtJHCgeoHY8UgogGyJ-jYXVUU7COyj83XDERC6g/s1600/IMG_8065.JPG
Azam FC
Yanga
MABINGWA wa soka wa Tanzania, Yanga pamoja na Mabingwa wa Kombe la Kagame, Azam jioni ya leo wanatarajia kuonyeshana undava wakati zitakapokutana kwenye mchezo wa Ngao ya Hisani.
Mchezo huo maalum kwa ajili ya kuzindua msimu mpya wa Ligi kuu ya Tanzania Bara utapigwa dimba la Taifa, huku timu zote zikitarajiwa kuwakosa baadhi ya nyota wake kutokana na matatizo mbalimbali.
Yanga ambao imeonyesha kuupania mchezo huo hasa baada ya kutolewa nishai na Azma kwenye robo fainali ya Kombe la Kagame, huenda isiwe na Amissi Tambwe aliyekuwa akisumbuliwa na Malaria, japo Donald Ngoma anaweza kucheza akitoka kuuguza maumivu ya nyonga.
Azam wenyewe wanaosaka ushindi wa kwanza wa mchezo huo wa Ngao ya Hisani na pia kujaribu kufuta uteja kwa wapinzani kila wakikitana kwenye pambano hilo inaweza kumkosa Kipre Tchetche.
Hata hivyo vikosi vyote chini ya makocha wao, Stewart Hall kwa Azam na Hans van Pluijm wa Yanga wamenukuliwa wakitamba kuwa leo itakuwa kazi tu, na kuzipa matumiani timu yao kushinda.
"Yanga ni wazuri na ni timu kubwa na unapocheza nao ni kama ina wachezaji 12 kutokana na mashabiki wanaoiunga mkono, lakini tupo tayari na vijana wanagu wana ari ya kushinda," alisema.
Pluijm alisema kuwa ameandaa vijana wake kwa ajili ya kazi moja ya kushinda Taifa, hasa baaada ya kuridhishwa na mabadiliko aliyoyaona kwa safu yake ya mbele wakiwa jijini Mbeya kwenye kambi.
Bila ya shaka mashabiki wa soka watapata uhondo katika mchezo huo utakaochezeshwa na mwamuzi Martin Saanya baada ya refa wa awali, Israel Nkongo kupatwa na dharura ya kuugua na kuenguliwa.
Rekodi Azam Ngao ya Hisani:
2012: Simba 3-2 Azam
2013 Azam 0-1 Yanga
2014: Yanga 3-0 Azam
2015: Azam v Yanga???

No comments:

Post a Comment