STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 21, 2015

3 zachemsha usajili Ligi Kuu Tanzania Bara 2015-2016

Stand United
Toto Africans
WAKATI dirisha la usajili kwa klabu vya Ligi Kuu nchini (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) likifungwa juzi klabu tatu za VPL vimeshindwa kuwasilisha usajili wao wa wachezaji katika muda uliopangwa.
 Akizungumza na wandishi wa habari leo, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) alivitaja Klabu za Coastal Union ya Tanga, Stand United ya Shinyanga na Toto African ya jijini Mwanza kuwa zimeshindwa kuwasilisha usajili wao na kusema faini ni 500,000  kwa mchezaji mmoja hivyo klabu iliyochelewesha usajili au itakayobadili majina au kuongeza majina baada ya usajili kufungwa italazimika kulipia faini
“Usajili umefungwa jana (juzi) na timu tatu hazijawasilisha usajili wao hata wa mchezaji mmoja pamoja na TFF kuongeza muda wa usajili kwa wiki mbili”, alisema Kizunguto
Pia alisema si kwamba timu zingine zimefikisha idadi ya wachezaji wote kulingana na kanuni bali zingine zimesajili wachezaji 18, 24 hivyo hata wao endapo wataongeza watalipia faini.
Kizuguto alikumbusha timu ambazo zimesajili wachezaji wa kigeni kuwasilisha ada zao ili waweze kupata kbali cha kucheza ligi.
Awali TFF ilitoa muda wa wiki mbili kwa vilabu vyote nchini kukamilisha usajili, ambapo vilabu 13 vya ligi kuu vimeweza kukamilisha ndani ya wakati, klabu 24 vya ligi daraja la kwanza, klabu 24 ligi daraja la pili pia vimeweza kukamilisha usajili wao ndani ya muda uliopangwa.


No comments:

Post a Comment