STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 21, 2015

Man United wakatwa maini kwa Sadio Mane

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2015/05/16/16/28BDB01200000578-3084365-Southampton_s_Sadio_Mane_celebrates_the_first_of_the_first_half_-a-3_1431789411065.jpgKLABU ya Southampton imekiri kuwa Manchester United wanamuwania winga wao wa kimataifa wa Senegal Sadio Mane, lakini ikatamka wazi kwamba mkali huyo hauzwi ng'o.
Wiki iliyopita Southampton walikanusha taarifa za kupokea ofa yeyote kwa ajili ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 23. Mshambuliaji wa Barcelona Pedro amekuwa akihisiwa kujiunga na United lakini kwa sasa yupo katika hatua za mwisho za kijiunga na Chelsea kwa dau la pauni milioni 21. 
Kutokana na hali hiyo United wameamua kuongeza nguvu zao katika kumsajili Mane kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili wa kiangazi. Mane amefunga mabao 10 katika mechi 32 alizocheza msimu uliopita baada ya kujiunga na klabu yake ya sasa akitokea Red Bull Salzburg ya Austria na yumo pia katika orodha ya wachezaji waliowahi kufunga magoli matatu -hat-trick kwa muda mfupi zaidi.
Hata hivyo mapema leo Ijumaa klabu hiyo ya Southampton imeweka bayana kwamba mchezaji huyo hauzwi hivyo Man United watafute pengine pa kupata mchezaji mpya.
Meneja wa The Saints, Ronald Koeman amefunguka kuwa mchezaji huyo hauzwi kwa bei yoyote.

No comments:

Post a Comment