STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 22, 2014

Chelsea, Arsenal vita tupu England

http://4.bp.blogspot.com/-F-hrxK9h4IU/UPq7uFio5yI/AAAAAAAAW1U/SYzNFu1Pn6w/s1600/Chelsea+vs+Arsenal+2013.jpg
PATASHIKA ya Ligi Kuu ya England inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo nane, huku macho na masikio ya mashibiki wa kandanda duniani kote wakifuatilia kwa karibu pambano la vinara wa ligi hiyo Chelsea itakayokuwa darajani kuikaribisha Arsenal.
Pambano hilo linavuta hisia za wengi kutokana na mchuano wao wa kuwania ubingwa msimu huu ambapo Arsenal wapo nafasi ya tatu ikizidiwa pointi nne na Chelsea na pia kuzidiwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa na Liverpool wanashika nafasi ya pili japo wanalingana pointi 62 kila mmoja.
Timu hizo zinakutana huku kukiwa na rekodi za kusisimua baina yao na hasa kwa makocha wao Jose Mourinho wa Chelsea na Arsene Wenger wa Arsenal.
Katika mechi 10 zilizokupita kwa makocha hao kukutana Mourinho amemtambia Wenger ambaye pambano hilo la leo litakuwa ni la 1,000 kwake tangu aanze kuinoa timu hiyo ya London ya Kaskazini.
Chelsea haijapoteza michezo 75 kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Stanford Bridge,  ingawa itaikabili Arsena yenye rekodi nzuri ya kushinda mechi za ugenini ikiwakosa wachezaji wake wa Kibrazil, Willian na Ramires walionyesha kadi nyekundu katika mechi yao iliyopita dhidi ya Aston Villa waliolazwa bao 1-0.
Mechi nyingine za ligi hiyo ni kama ratiba inavyoonyesha hapo chini.
18:00 Cardiff V Liverpool
18:00 Everton V Swansea
18:00 Hull V West Brom
18:00 Man City V Fulham
18:00 Newcastle V Crystal Palace
18:00 Norwich V Sunderland
20:30 West Ham V Man United

Kesho Machi 23
16:30 Tottenham V Southampton
19:00 Aston Villa V Stoke

No comments:

Post a Comment