STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 22, 2014

Man Ud kuivaa Bayern bila van Persie, Chelsea vs PSG

Taji linalowaniwa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya
Manchester Utd wakishangilia moja ya mabao matatu yaliyowavusha robo fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya
MABINGWA watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bayern Munich imepangwa kukutana na Mabingwa wa England, Manchester United katika mechi za Robo Fainali ya michuano hiyo huku Chelsea ikipangiwa kuumana na PSG ya Ufaransa.
Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo iliyopigwa droo yake Nyon, Uswisi,  timu mbili kati ya tatu zinazofukuzana kwenye Top 3 ya Ligi ya Hispania, Barcelona na Atletico Madrid zitakuna a zenyewe kwa zenyewe huku Real Madrid itamenyana na Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Manchester Utd iliyopenya bila kutarajiwa kwenye hatua hiyo ni kama imepewa kazi ya kupanda mlima mrefu mbele ya Bavarian ambao wapo kwenye kiwango cha hali ya juu msimu huu tofauti na Mashetani Wekundu ambao wanasuasua chini ya kocha David Moyes.
Kibaya zaidi itavaana na watetezi hao bila ya nyota wao, Robin van Persie aliyeumia wakati akiivusha timu hiyo hatua hiyo na atakayekaa nje kwa wiki karibu sita.

Hatua hiyo inatarajiwa kucheza kati ya April 1-2 kwa mechi za mkondo wa kwanza kabla ya marudiano kufanyika Aprili 8 na 9.
 

Ratiba kamili ipo hivi:Barcelona vs Atletico Madrid
Real Madrid vs Borussia Dortmund
Paris Saint-Germain vs Chelsea
Manchester United vs Bayern Munich

No comments:

Post a Comment