STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, January 5, 2015

Lukas Podolski awashukuru Arsenal akitua San Siro

http://cdn.caughtoffside.com/wp-content/uploads/2014/12/460208232.jpg
Lucas Podolski
MPANGO wa Lukas Podolski kuhamia Inter Milan kwa asilimia kubwa umekamilika kufuatia  mshambuliaji huyo wa Ujerumani kukutana na kocha wa klabu hiyo Roberto Mancini katika uwanja wa mazoezi wa timu hiyo Jumamosi.
Nyota huyo ameshaaga Arsenal tayari kuanza maisha mapya katika Ligi ya Italia maarufu kwa jina la Seria A.
“Mshindi huyu wa kombe la dunia alikuwepo Centro Sportivo Angelo Moratti leo (jana) kwa lengo la kufahamu uwanja wake mpya wa mazoezi na alikutana na kocha wa Nerazzurri ,” taarifa ya Inter Milani kwa vyombo vya habari ilieza.
Mshambuliaji huyo wa Gunners amecheza mechi 13 tu za michuano yote msimu huu, hakuna aliyoanzishwa, lakini bado alitumia muda wake kuwashukuru mashabiki kwa sapoti yao kuelekea kuondoka kwake.
“Siwezi kuelezea kwa maneno shukrani yangu kwa mashabiki wa Arsenal kwa yote waliyoyafanya kwangu katika miaka yangu niliyokuwapo London,” aliandika katika ukurasa wake wa Instagram.
“Tafadhalini mtambue kuwa moyo wangu daima una nafasi yenu. Natumai nimeacha alama yangu klabuni na kwa mashabiki pia. Natumai tutaonana tena! COYG.”
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na Arsenal akitokea FC Koln 2012 na mkataba wake wa sasa na Gunners unamalizika Juni 2016.

No comments:

Post a Comment