STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, October 13, 2013

Mauaji!: Mtangazaj ITV/Radio One apigwa risasi, ampoteza mama mzazi

Ufoo Saro (kulia) aliyepatwa na mkasa hivi punde
HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema mtangazaji wa kituo cha ITV, Ufoo Saro amejeruhiwa vibaya kwa risasi, huku mama yake mzazi akipoteza maisha baada ya mtu anayedakiwa kuwa mchumba wake au mumewe kuwafyatulia risasi katika ugomvi wa kimapenzi.

Taarifa zinasema kuwa mchumba wa mtangazaji huyo aliyetajwa kwa jina la Ansel aliyekuwa nchini Sudan kikazi alitua nchini jana na kufikia kwa Ufoo lakini kukatokea mzozo ambao haukupata suluhisho.

Hivyo wawili hao waliongozana hadi kwa mama wa mtangazaji huyo kutafuta suluhu, asubuhi hii na kwa bahati mbaya hali ilikuwa tete na ndipo kijana huyo alipotoa bastola aliyokuwa nayo na kumtwanga mama mtu risasi ya kichwa iliyomuua papo hapo.

Kama hiyo haikutosha inaelezwa jamaa huyo alimtwanga risasi Ufoo kifuani na nyingine mguuni na kudhani amemuua kabla ya yeye mwenyewe kujilipua mwenyewe kwa risasi ya kidevuni na kumuua.

Tayari miili ya watu hao wawili yaani mama yake Ufoo na jamaa huyo imepelekwa Muhimbili sambamba na mtangazaji huyo anayeelezwa yupo katika hali mbaya kwa ajili ya kuhifadhiwa na matibabu zaidi.

Haifahamiki chanzo cha mauaji hayo licha ya kudaiwa huenda ni ugomvi wa kimapenzi na haifahamiki jamaa huyo huko Sudan anakodaiwa kuwa alikuwa akifanya kazi UN alikuwa kama nani japo inaelezwa huenda alikuwa mwanajeshi ambapo kabla ya kwenda huko aliwahi kuwa mpiga picha wa ITV na kufanya kazi Mahakama ya Kimataifa ya Arusha kabla ya kuomba kazi UN.
MICHARAZO inaendelea kufuatia kwa kina taarifa hii na itawafahamisha. Pia inamuombea kila la heri na salama mtangazaji huyo aweze kupona katika mkasa uliopata na kumpoa pole kwa msiba uliompata kwa kumpoteza mama yake mzazi.

No comments:

Post a Comment