STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 20, 2014

Liverpool majanga! Yazamishwa 3-1 na West Ham

Winston Reid (r)
West Ham wakiiadhibu Liverpool

Winston Reid
Bao la kwanza la West Ham likitumbukizwa wavuni na Winston Reid kwa kichwa
Diafro Sakho (second on the left)
West Ham wakishangilia bao lao la pili lililofungwa na Diafro Sakho
Mario Balotelli and Adrian
Balotelli akikoromewa na kipa wa West Ham
Raheem Sterling (l)
Sterling akipongezwa baada ya kufunga bao la kufutia machozi la Liverpool
TIMU ya Liverpool wameendelea kuwa urojo katika Ligi Kuu ya England baada ya mudfa mfupi uliopita kunyukwa mabao 3-1 na West Ham United katika pambano kali lililochezwa Upton Park.
Liverpool ambayo wiki iliyopita ilinyukwa nyumbani na Aston Villa kwa bao 1-0, ilishindwa kupata dawa ya kurejea kwenye makali yake ikiwa haina Luis Suarez baada ya kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa mabao 2-1.
Winston Reid aliwaandikia wenyeji bao dakika ya pili tu ya mchezo akimalizia kazi ya Tomkins kabla ya Diafro Sakho kuongeza la pili dakika tano baadaye na kuwapa presha vijana wa Branden Rodgers kuepuka kipigo ugenini.
Juhudi zao zilizaa matunda dakika ya 26 wakati Raheem Starling kufunga bao la pekee la timu yake, hata dakika za lala salama wenyeji waliandika bao la tatu lililowafanya Liverpool iliyotoka kupata ushindi wa mabao 2-1 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kushindwa kuepuka kipigo hicho kwa West Ham baada ya  Morgan Amalfitano kusukumua mpira wavuni akimalizia kazi nzuri ya Stewart Downing.

No comments:

Post a Comment