STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, September 20, 2014

Tanzania yazidi kuporomoka FIFA, Cameroon yapaa

http://imikinonews.com/files/news_images/1596757601114051870520140716101415.jpgTANZANIA imeendelea kuporomoka tena kwenye viwango vya soka vinavyotolewa kila mwezi na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), baada ya kuanguka kwa nafasi tano katika viwango vipya vilivyotolewa.
Tanzania, ambayo ilifungwa 2-0 na Burundi katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyopita, sasa inakamata nafasi ya 115 duniani na 33 barani Afrika ikiwa nyuma ya Uganda wanaoongoza Afrika Mashariki wakiwa nafasi ya 79 duniani na 19 Afrika, Rwanda walioko nafasi ya 93 duniani na 25 Afrika na Kenya walioporomoka kwa nafasi saba wakiwa nafasi ya 30 Afrika na 111 duniani.
Aligeria waliopanda kwa nafasi nne, wanaongoza barani Afrika wakiwa nafasi ya 20 duniani wakifutwa na Ivory Coast walioshuka kwa nafasi tatu baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Cameroon waliopanda kwa nafasi 12 na kukamata nafasi ya nane Afrika na 42 duniani.
Nafasi ya tatu barani Afrika inakaliwa na Tunisia (31) wakipanda kwa nafasi 11 wakifuatwa na Ghana (33), Senegal (36), Nigeria (37) na Cape Verde (41). Guinea waliopanda kwa nafasi 16 wanakamata nafasi ya tisa barani Afrika na 48 duniani huku Burkina Faso waliopanda kwa nafasi 10 wakifunga pazia la 10 bora barani Afrika wakifungana na Guinea katika nafasi ya 48 duniani.
Uganda pia ni wa kwanza katika Ukanda wa Cecafa wa Afrika Mashariki na Kati wakifuatwa na Rwanda, Kenya, Tanzania, Burundi, Ethiopia (39, 132), Sudan (40, 133), Shelisheli (47, 172), Sudan Kusini (50, 185), Eritrea (52, 202), Somalia (53, 204) huku Djibouti wakifunga mlango Cecafa na Afrika wakiwa 54 Afrika na 205 duniani.
Mabingwa wa dunia, Ujerumani wanaongoza 10 bora ulimwenguni wakifuatwa na Argentina, Colombia waliopanda kwa nafasi moja wakiwashusha Uholanzi, Ubelgiji, Brazil, Uruguay, Hispania, Ufaransa na Uswis.

No comments:

Post a Comment