STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 21, 2014

Tevez aiangamiza AC Milan Italia

Carlos Tevez
Carlos Tevez akitupia kitu nyavuni na kuwaacha kipa na mabeki wa Milan wakiwa katika simanzi
BAO pekee lililofungwa na Muargentina, Carlos Tevez katika dakika ya 71 akimalizia kazi ya Paul Pogba lilitosha kuwapa ushindi mujarabu mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Italia, Seria A Juventus dhidi ya AC Milan katika pambano lililochezwa uwanja wa San Sirro, mjini Milan.
Kipigo hicho kimeishusha Milan mpaka nafasi ya tatu ikisaliwa na pointi zake 6 na kuwapisha Juventus kukaa kileleni ikiwa na pointi 9 na mabao manne ya kufungwa ikiwa haijafungwa bao lolote mpaka sasa.
AS Roma waliokuwa nafasi ya tatu wamepanda hadi nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa dhidi yake na Milan ambao wamefunga mabao nane na kuruhusu mabao sita.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo mbalimbali ambapo mapame saa saba mchana huu, Chievo Verona itakuwa nyumbani kuialika Parma, Genoa itaialika Lazio na AS Roma watakuwa nyumbani kuikaribisha Cagliari.
Mechi nyingine za leo ni kati ya Sassuolo dhidi ya Sampdoria, Atalanta itaikaribisha Fiorentina, Udinese itaialika Napoli, Palermo itakuwa wenyeji wa Inter Milan na Hellas Verona watakuwa wageni wa Torino.

No comments:

Post a Comment