Adebayor akipaparika kuisaidia Spurs isife nyumbani bila mafanikio |
Hivi ndivyo Mashetani Wekundu walivyonyonyolewa leo ugenini na Leicester City |
Manchester iliyofanya 'mauaji' ya kutisha wiki iliyopita kwa kuifumua timu kibonde ya QPR kwa mabao 4-0 ilionekana kama ingeendeleza ushindi kwa Leicester City baada ya kutangulia kupata mabao mawili ya haraka.
Mabao hayo yaliyofungwa na Robin van Persie katika dakika ya 13 ya mchezaji akimalizia kazi nzuri ya Radamel Falcao na Angel di Maria kuongeza la pili dakika tatu baada ya kumegewa pande na Wayne Rooney.
Hata hivyo hilo la pili halikudumu kwani dakika moja baadaye Ulloa aliifungua wenyeji bao na kufanya matokeo kuwa 2-1 hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili Mashetani Wekundu ambao wana pengo katika nafasi ya ulinzi tangu walipowauza Rio Ferdinand na Namanja Vidic, waliongeza bao la tatu dakika ya 57 na kiungo Ander Herrera kwa kazi nzuri ya Di Maria.
Wenyeji walicharuka na kurejesha bao la pili dakika ya 62 kwa mkwaju wa penati kupitia Nugent kabla ya Cambiasso kusawazisha bao dakika mbili baadaye, huku pia Mashetani Wekundu wakimpoteza beki wao Blackett kwa kadi nyekundu.
Magoli yaliyoizamisha vijana wa Louis Van Gaal, yalitumbukizwa wavuni katika dakika ya 79 na Vardy na Ulloa akahitimisha kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 83.
Katika mechi nyingine iliyochezwa mapema sambamba na pambano hilo, Spurs ikiwa nyumbani iliendeleza uteja baada ya kulazwa bao 1-0 na wageni wao West Brom.
Bao lililoiua Spurs lilifungwa na James Morrison katika dakika ya 74, licha ya wenyeji kucharuka kutaka kuondokana na aibu ya kulala nyumbani.
Ligi inaendelea kwa mechi mbili kati ya Crystal Palace dhidi ya Everton na Manchester City dhidi ya Chelsea.
No comments:
Post a Comment