BONDIA
Yohana Mathayo 'Tembo Mtoto' amefariki dunia jioni ya jana akiwa
mazoezini kwake eneo la Kigogo Mburahati Dar es Salaam.
Kifo hicho
kilimkuta ghafla wakati akifanya mazoezi ya kujiandaa na mpambano
wake wa ubingwa uliopangwa kufanyika hivi karibuni.
Taarifa za kifo cha bondia huyo aliyekuwa akizidi kupanda chati nchini miongoni mwa mabondia vijana, zilitolewa na kocha wake Kwame Mkuruma, aliyedai mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwao Manzese na
huenda akasafilishwa kwenda kuzikiwa kwao mkoa wa Tanga.
Mungu ametoa na Mungu ndiye aliyetwaa. Roho yake ilale mahali pema ila Yohana Mathayo 'Tembo Mtoto' utakumbukwa daima na wadau wenzako wa ngumi umetangulia nasi tu nyuma yako.
Bondia huyo mwenye rekodi ya kucheza
michezo 7 ya ngumi za kulipwa akiwa ameshinda mara 4 na kupigwa mara
moja na droo mara mbili. Marehemu huyo enzi za uhai wake alijiunga na ngumi za kulipwa mwaka 2011
ambapo mchezo wake wa kwanza kacheza na Seba Temba wa Morogoro ambapo
alitoa nae droo na mchezo wake wa mwisho kucheza ni Agosti 9 mwaka huu ambapo alishinda kwa TKO ya raundi ya pili dhidi ya Shujaa Keakea.
No comments:
Post a Comment