STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, April 11, 2014

Sevilla, Valencia, Juve, Benfica hizoo nusu fainali Europa League

Pirlo kati akipongezwa na wenzake kwa kufunga bao la kuongoza
Sevilla walipokuwa wakiinyoosha Porto
KLABU za Hispania zimeendelea kung'ara Ulaya baada ya jana Valencia na Sevilla kupindua matokeo na kufuzu Nusu Fainali ya Ligi Ndogo ya Ulaya (Europa League) dhidi ya Basel na Porto, huku mabingwa watetezi wa Italia, Juventus nao wakitinga hatua hiyo kwa kuibamiza Olymnpique Lyon.
Valencia iliyokuwa imetandika mabao 3-0 na Basel iliitupa nje timu hiyo ya Uswisi baada ya kuwacharaza mabao 3-0 na kuingi kwenye muda wa nyongeza na kushinda mabao mawili ya ziada na hivyo kufua Nusu Fainali kwa kishindo cha mabao 5-3, huku ndugu zao wa Sevilla waliolala 1-0 katika mechi ya kwanza iliishindilia Porto ya Ureno mabao 4-1 na kufuzu kwa jumla ya mabao 4-2.
Katika mechi ya Juventus iliyoshinda mechi ya ugenini bao 1-0, ilianza kuwashutua wageni wao kwa kuwatangulia kwa bao la mapema la dakika ya nne lililofungwa na Andre Pirlo kabla ya Jimmy  kusawazisha katika dakika ya 18 akimalizia kazi nzuri ya Mvuemba.
Hata hivyo katika dakika ya 68 Samuel Umtiti alijifunga bao katika harakati za kuokoa shambulizi langoni mwake na kuiwezesha Juve kushinda mabao 2-1 na kusonge mbele kwa mabao 3-1.
Katika mechi nyingine ya marudiano ya robo fainali ya michuano hiyo, AZ ya Uholanzi ilishindwa kutamba mbele ya Benfica ya Ureno baada ya kufungwa mabao 2-0 na hivyo kungoka kwa jumla ya mabao 3-0.
Mabao ya wenyeji yalipachikwa wavuni katika kipindi na mshambuliaji wake nyota Rodrigo katika dakika ya 39 na 71 yote yakitokana na pasi za Salvio.
Washindi hao watasubiri kujua wataumana na nani katika droo inayotarajiwa kutolewa leo kama itakavyokuwa kwa ile ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo Hispania imetoa timu mbili Real Madrid na majirani zao Atletico Madrid, watetezi Bayern Munich na Chelsea ya England.

No comments:

Post a Comment