STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 15, 2014

Ratiba ya Ligi ya Mabingwa hii hapa


KLABU ya Manchester City imepangwa kucheza na Barcelona katika hatua ya mtoano ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika ratiba iliyopangwa leo jijini Nyon, Ufaransa. 
Timu hizo zilikutana pia katika hatua hiyo msimu uliopita ambapo Barcelona waliibuka na ushindi wa jumla ya mabao 4-1 na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. 
Timu zingine ambazo zilikutana msimu uliopita katika hatua hiyo ni pamoja na Paris Saint-Germain ambao watakwaana tena na Chelsea msimu huu. 
Wengine ni mabingwa watetezi Real Madrid ambao watakwaana na Schalke wakati mshindi wa pili msimu uliopita Atletico Madrid wao wataivaa Bayer Leverkusen. 
Mabingwa wa Serie A Juventus wao watawakaribisha Borussia Dortmund huku mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wakicheza na Shakhtar Donetski, Arsenal wenyewe watacheza na Monaco na Porto watakwaana na FC Basel. 
Timu ambazo zilimaliza katika nafasi ya pili katika hatua ya makundi zitacheza mechi zao za kwanza nyumbani kati ya Februari 17/18 na 24/25 huku zile za marudiano zikitarajiwa kuchezwa kati ya Machi 10/11 na 17/18.

No comments:

Post a Comment