STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, September 1, 2014

TFF ya Malinzi yaanza kumeguka, Mtawala abwaga Manyanga

http://4.bp.blogspot.com/-EzqgYESEWrk/Url0Uwr3IUI/AAAAAAAAJuU/Sh3M7Bv08bw/s1600/DSC_0392.JPG
Evodius Mtawala (kulia) akiwa na viongozi wenzake wa TFF kabla ya kubwanga manyang'a
TAARIFA zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa, aliyekuwaMkurugenzi wa wa Vyama na Masuala ya Kisheria katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Evodius Mtawala, ameachia ngazi katika nafasi hiyo.
Inaelezwa kuwa
Mtawala Katibu Mkuu huyo wa zamani wa Simba,  alikuwa na hali ya kutokuelewana na uongozi wa shirikisho hilo na ndiyo chanzo cha kung'atuka TFF.
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa, alithibitisha kuachia ngazi kwa Mtawala lakini akasema ni kutokana na sababu mbalimbali za taaluma yake ya uanasheria.
“Ni kweli Mtawala hataendelea kufanya kazi TFF lakini ameamua kuchia ngazi mwenyewe kutokana na sababu mbalimbali alizodai kwamba ni kujikita na taaluma yake zaidi kwa sasa, lakini mambo mengine juu ya hilo yatabaki kuwa siri baina yake na mwajiri wake.
“Ila mpaka makubaliano ya mwisho yalieleza kuwa itakapofika mwisho wa mwezi wa nane (jana 31, Agosti) atakuwa tayari ameshakabidhi ofisi na kuendelea na masuala ambayo alidai anahitaji kujikita zaidi kulingana na taaluma yake,” alisema Mwesigwa.
Mtawala amedumu kwenye wadhifa huo kwa miezi nane tu tangu alipoteuliwa Desemba 24, mwaka jana chini ya uongozi wa rais mpya, Jamal Malinzi. 

No comments:

Post a Comment