STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 1, 2016

Jerome Boateng afarijika na kumshukuru Kansela Merkel

https://blog-blogmediainc.netdna-ssl.com/upload/SportsBlogcom/4259301/0335206001446232183_filepicker.jpg
Jerome Boateng
http://i0.web.de/image/406/31373406,pd=3/alexander-gauland-afd.jpg
Alexander Gauland aliyetoa kauli za kibaguzi dhidi ya Jerome Boateng
KIROHO safi. Beki wa kimataifa wa Ujerumani, Jerome Boateng amedai kuwa ubaguzi nchini humo bado upo kwa kiasi kikubwa, ila ameshukuru namna Kansela Angela Merkel kwa jinsi alivyoiponda vikali kauli iliyotolewa na mwanasiasa anayeheshimika nchini humo, Alexander Gauland.
Gauland alikaririwa mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa asingependa kuwa rafiki au hata jirani na nyota huyo wa Bayern Munich ambaye ana asili Ghana.
Kauli hiyo ilizua mjadala mkubwa huku ikipondwa vikali na watu mbalimbali akiwemo Afisa Mkuu wa Ligi ya Soka ya Ujerumani-DFL aliyedai kuwa kauli hiyo mbaya na isiyovumilika.
Msemaji wa Kansela Merkel amesema 'bosi' wake amesikitishwa sana na kauli hiyo ikizingatiwa kuwa imetoka kwa mwanasiasa huyo anayeheshimika.
Boateng akihojiwa kuhusiana na suala hilo alisema amefarijika mno kuona watu mbalimbali wanavyopingana na kauli hiyo akiwemo kansela Merkel na kuongeza kuwa vita vya kupambana na ubaguzi wa rangi bao haijaisha.

No comments:

Post a Comment