STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 1, 2016

Yanga yaipoka TFF uchaguzi mkuu wao kufanyika Juni 11

http://2.bp.blogspot.com/-2jspLbxdTC4/VqjXv-Gxl_I/AAAAAAAACAg/oYANqZloaFI/s1600/yanga.JPGWAKATI Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iliyopewa jukumu la kusimamia uchaguzi wa Yanga ikiongeza muda wa uchukuaji na urudishwaji fomu za uchaguzi huo, uongozi wa mabingwa hao wa soka umeamua kuonyesha ubabe.
Uongozi huo umetangaza kutoutambua uchaguzi huo wa Juni 25 na badala yake kuutangaza wao ambao utafanyika Juni 11 na zoezi la uchukuaji fomu za uchaguzi huo utakaoshirikisha wanachama wote wakiwamo wa zamani na wale wenye kadi za Benki ya Posta.
Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Baraka Deusdedit, alitangaza maamuzi hayo leo kwa madai kuwa, TFF haiwezi kuusimamia uchaguzi wao kwa vile hawawajui wanachama halali wa klabu hiyo.
Baraka alisema kuwa, wanaweza kuwekewa mamluki na kuivuruga Yanga ambayo kwa siku za karibuni imekuwa na mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi kiasi cha kutinga hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni rekodi kwa klabu za Ukanda wa Afrika Mashariki na Tanzania kwa ujumla.
Uongozi huo umesema zoezi la kuchukua na kurudisha fomu litaanza kesho Juni 2-3 kabla ya kufanyiwa usaili na baadaye kuendelea na taratibu nyingine ikiwamo pingamizi na kisha kuwasilisha majina ya wagombea watakaopitishwa kabla ya kampeni kuanza Juni 8-10 na uchaguzi kufanyika Juni 11 kisha matokeo yake kutangazwa Juni 12.
Hata hivyo hayo yanaendana kinyume na Kamati ya Uchaguzi wa TFF inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Wakili Msomi Alloyce Komba kutokana na mipango yake, imesogeza mbele mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu mpaka Jumatatu Juni 6, 2016 saa 10:00 jioni. Isipokuwa Jumamosi na Jumapili ya Juni 4 na 5, 2016.

Mpaka jana wanachama tisa (9) walikuwa wamechukua na kurejesha fomu. Wanachama hao ni Aaron Nyanda na Titus Osoro wanaowania nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2010 inayotambulika serikalini hadi sasa.

Wengine ni Paschal Laizer, Edgar Chibula, Mohammed Mattaka, Mchafu Ahmed Chakoma, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ Omari Said kutoka Zanzibar ambao wanawania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji. Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Juni 25, 2016.

Fomu zinapatikana katika ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam. Vilevile utaratibu unafanyika ili fomu ziweze kupatikana katika tovuti ya shirikisho www.tff.or.tz


Fomu zinapatikana kwa gharama ya Sh 200,000 kwa 

nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti na Sh 

100,000 kwa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa 

kamati ya utendaji.  

No comments:

Post a Comment