STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, March 2, 2015

El Merreikh yamfukuzisha kazi kocha wa Azam

http://jamboleo.co.tz/wp-content/uploads/2014/12/OMOG.jpg
MABINGWA wa soka nchini, Azam imemtimua kocha wake, Joseph Omog na msaidizi wake Ibrahim Shikanda na baadhi ya watendaji baada ya klabu hiyo kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katibu Mkuu wa Azam, Idrissa Nassor 'Father' ameweka bayana maamuzi hayo akisema imetokana na makubaliano waliyowekeana na Mcameroon huyo wakati wakiingia naye mkataba.
Father alisema kuwa, wakati wanaingia mkataba na Omog walikubaliana kuivusha mahali ilipo Azam ikiwamo kufanya vema kwenye michuano ya kimataifa, lakini kwa miaka miwili kocha huyo ameshindwa.
"Kwa hali hiyo tumeamua kuachana kwa wema na yeye mwenyewe analifahamu hilo, na hajatoka pekee yake bali na msaidizi namba mbili Ibrahim Shikanda na baadhi ya watendaji wa benchi la ufundi,"alisema.
Aliongeza kuwa kwa sasa timu itakuwa chini ya Kocha msaidizi  kutoka Uganda, George Nsimbe ambaye atakaimua nafasi hiyo mpaka watakapopata kocha mkuu katika mchakato utakaoendeshwa na klabu yao.

No comments:

Post a Comment