STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, August 25, 2014

Kinyambe aamua kuanzisha kampuni Mbeya

http://2.bp.blogspot.com/-nD77bTwFV0U/UtAO8K2MlmI/AAAAAAAAHNg/re3SC9j9Mas/s1600/1521701_579327915475733_414873147_n.jpg
Kinyambe kushoto, alipokuwa Vituko Show akiwa na mpiga picha Yosso Komando
MCHEKESHAJI maarufu nchini James Mohammed 'Kinyambe' ameanzisha kampuni yake ya kutengeneza filamu iitwayo Kinyambe Video Production ambayo ipo njiani kuachia kazi ya kwanza iitwayo 'Fumbafu Thana', huku akimaliza nyingine jijini Mbeya.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka kambini Mbeya, Kinyambe alisema kampuni hiyo ambayo inadili na kutengeneza filamu na video za muziki, itakuwa ikisaidia wasanii chipukizi wa mkoani humo na kwingineko ambao watakuwa wakihitaji kuendeleza vipaji vyao.
Kinyambe aliyejipatia umaarufu mkubwa kwa staili yake ya kuigiza kama zezeta na kuyabadilisha macho yake kama kinyonga, alisema filamu ya 'Fumbafu Thana' ilitengenezwa mapema, lakini ilikwama kutokana ambapo sasa itaachiwa mapema mwezi ujao.
Alisema wakati filamu hiyo ikiwa njiani kutoka, pia ameshaanza kutengeneza filamu nyingine aliyoigiza na wasanii chipukizi wa jijini Mbeya akiwamo Deus Luis aliyewahi kuuza sura na marehemu Steven Kanumba katika filamu ya 'Poison Leather'.

No comments:

Post a Comment