STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, August 25, 2014

Juma Luizio 'Ndanda' achekelea maisha mapya Zesco

http://images.uncova.com.s3.amazonaws.com/fad774132f9c41bc2ebfb8ec3a7a75a625cd45e6.jpg
Juma Luizio akiwa kwenye mazoezi ya timu ya Zesco nchini Zambia
MSHAMBULIAJI chipukizi wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya ZESCO ya Zambia, Juma Luizio 'Ndanda', amesema hakuna kitu kinachomstaajabisha ugenini kama viwanja vya mazoezi vya timu.
Ndanda anayeichezea pia timu ya taifa aliyetua Zesco akitokea Mtibwa Sugar alisema klabu za Zambia zinajitahidi mno kuwa na viwanja vya mazoezi tofauti na ilivyo nyumbani Tanzania.
Akizungumza na MICHARAZO kwa njia ya mtandao mapema leo asubuhi, mchezaji huyo alisema mazingira mazuri aliyokutana nayo Zambia yamemfanya kujisikia faraja.
"Dah mazingira ya huku fresh sana kaka wametuzidi sana kwa sababu kwamba ni waelewa wanaojua nini maana ya mpira, pili wanawalipa vizuri wachezaji pia kuhusu viwanja dah! Aisee kila timu wamejitahidi kuwa na uwanja wa mazoezi na mechi tena vizuri tofauti na huko," alisema.
Luizio aliyemaliza msimu uliopita akiwa mmoja wa wafungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, alisema kwa kipindi kifupi tangu atue Zesco aliyoingia mkataba wa miaka mitatu ameyazoea mazingira ya soka la nchini hiyo.
"Nashukuru sana nimeshazoea maisha ya huku na naahidi kuitangaza vyema nchi yangu nikiwa na ndoto za kupata nafasi ya kucheza soka Ulaya," alisema.

No comments:

Post a Comment