STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, August 25, 2014

Meya Kinondoni kuzindua ngumi za 10 Bora J'mosi

http://www.ippmedia.com/media/picture/large/mwenda-july19-2013.jpg
MEYA wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi na kuyazindua mashindano ya ngumi za ridhaa za mkoa wa Dar es Salaam yatakayoanza Agosti 30.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Chama cha Ngumi za Ridhaa Mkoa wa Dar es Salaam (DABA) yanafahamika kama Kumi Bora na yataendeshwa kwa muda wa miezi miwili kabla ya kufikia tamati Novemba 30.
Afisa Habari wa DABA, Mwamvita Jacob aliiambia MICHARAZO kuwa michuano hiyo itafanyika kwenye ukumbi wa Manyara uliopo Tandele CCM na siku ya ufunguzi Meya wa Mwenda ndiye atakayekuwa mgeni rasmi.
Mwamvita alisema michuano hiyo itashirikisha klabu zote za ngumi za ridhaa za mkoa wa Dar es salaam.
"DABA inatarajia kuendesha mashindano ya ngumi ya Kumi Bora ambayo yatazinduliwa rasmi siku ya Jumamosi na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda majira ya saa 10 na yatafikia tamati Novemba 30," alisema. Mwamvita alisema michuano hiyo itatumika pia kusaidia mikoa ya kimichezo ya Ilala, Temeke na Kinondoni kupata timu za kuziwakilisha kwenye mashindano ya taifa ya ngumi itakayofanyika Oktoba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment