STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 29, 2013

'Bondia Ibrahim Maokola hajakamatwa, katelekezwa Italia'

https://fbcdn-sphotos-f-a.akamaihd.net/hphotos-ak-ash3/944257_379837705469127_1264255997_n.jpg
Bondia Ibrahim Maokola
 KOCHA wa bondia machachari wa ngumi za kulipwa nchini, Ibrahim Maokola, Chaurembo Palasa amekanusha taarifa kwamba bondia huyo amekatwa nchini Italia kwa tuhuma za dawa za kulevya.
Badala yake Palasa alisema Maokola, aliyechukuliwa na promota maarufu nchini Shomari Kimbau ametelekezwa na promta huyo akiwa hana tiketi ya kurejea nchini.
Palasa alisema bondia wake alichukuliwa kinyemela na Kimbau kwenda kupigana na mipango ikaenda hovyo na Kimbau kumtoroka na kumuacha akiwa hana msaada wowote mpaka sasa na siyo kweli kama katiwa mbaroni kwa tuhuma za dawa za kulevya kama ilivyoelezwa na gazeti moja la kila wiki.
"Bondia Ibrahim Maokola, hajakamatwa Italia kama ilivyoripoti gazeti la ....la wiki iliyopita. Bondia Maokola alichukuliwa na Shomari Kimbau kwenda kupigana ngumi Italia mpaka muda huu bondia huyo ametelekezwa ghetto akiwa hana tiketi ya kurudi Tanzania," Palasa aliiambia MICHARAZO.
Awali ilielezwa kuwa bondia huyo na promota huyo walinaswa Italia kwa tuhuma kwamba walipeleka dawa za kulevya, ingawa hakuna uthibitisho wowote uliowahi kutolewa kuthibitisha taarifa hizo na hivyo meneja huyo wa Maokola ameamua kuweka sawa ili kusafisha hali ya hewa ambayo ilianza kumchafukia bondia wake wakati yupo kwenye matatizo, yeye akijaribu kuwasiliana na familia yake ili kumsaidia arejee nchini..

No comments:

Post a Comment