STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 29, 2013

Vijana wa Mbwana Makatta nouma, Prisons aibu tupu!

JKT Ruvu
MAAFANDE wa JKT Ruvu, timu inayonolewa na kocha Mbwana Makatta ndiyo timu pekee ambayo haijaruhusu wavu wake kutikiswa katika Ligi Kuu Tanzania Bara iliyoingia kwenye mapumziko mafupi kupisha maandalizi ya pambano la kimataifa kati ya Tanzania na Gambia.
Kadhalika timu ndiyo pekee iliyopata ushindi mfululizo miongoni mwa timu 14 zinazoshiriki ligi hiyo iliyoanza mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo imeshuhudiwa jumla ya mabao 32 yakiwa yamefungwa katika mechi 14 mpaka sasa.
JKT iliyokuwa na msimu mbaya ligi iliyopita, ilianza kwa ushindi wa mechi mbili mfululizo kwa kuzilaza Mgambo JKT kwa mabao 2-0 kabla ya kuisulubu Prisons ya Mbeya kwa mabao 3-0 jana na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiiengua Yanga waliokuwa wakiongoza kwa uwiano wa mabao ya kufunga.
Vijana hao wa kipa huyo wa zamani wa Tukuyu Stars na Yanga, inaongoza ikiwa na pointi 6 na mabao matano ikiwa haijatikiswa wavu wake, huku Yanga wakiteremka hadi nafasi ya pili wakiwa na pointi zake nne sawa na timu nyingine tano za Azam, Coastal Union, Simba, Mbeya City na Mtibwa Sugar.
Wakati JKT ikiwa haijafungwa bao hata moja, Prisons ndiyo inayoonekan timu yenye ngoma dhaifu ikiwa imeruhusu mabao sita ikiwa yenyewe haijafunga bao lolote katiia mechi zake mbili ilizocheza, ingawa mchezaji wau Lauriani Mpalile alijifungwa katika pambano lao la kwanza dhidi ya JKT walipolala 3-0.
Ashanti United wanafuatia kuwa na ngome dhaifu ikiwa imeruhusu pia mabao sita japo wenyewe wana bao moja walilopata walipocharazwa mabao 5-1 na Yanga Jumamosi iliyopita, ambapo wao Prisons na JKT Oljoro ndizo timu pekee ambazo hazijaonja pointi hata moja baada ya timu zote kucheza mechi mbilimbili.
Oljoro jana ilikubali kulala 1-0 kwa Simba baada ya kupoteza kwa mabao 2-0 mbele ya Coastal katika mechi ya ufunguzi wa ligi na kuwa timu yenye safu butu ya ushambuliaji kama ilivyo kwa Kagera Sugar na Prisons ambazo hazijapata bao mpaka sasa.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea Septemba 14 kwa mechi kadhaa, lakini baada ya mechi za jana msimamo kamili wa ligi hiyo upo kama ufuatavyo na wafumania nyavu orodha yao ipo chini ya msimamo huo;

                               P  W  D  L  F  A  GD  Pts
JKT Ruvu               2    2   0   0  5  0   5     6
Yanga                     2    1   1   0  6  2   4     4
Azam                      2    1   1   0  3  1   2     4
Coastal Union         2    1   1   0  3  1   2     4
Simba                     2    1   1   0  3  2   1     4
Mbeya City             2    1   1   0  2  1   1     4
Mtibwa Sugar         2    1   1   0  2  1   1     4
Ruvu Shooting         2    1   0   1  4  2   2    3
Mgambo                 2    1   0   1   1  2  -1   3
Rhino Rangers        2     0   1   1   2  4  -2   1
Kagera Sugar         2     0   1   1   0   1  -1   1
Oljoro                    2     0   0   2   0   3  -3   0
Ashanti                   2     0   0   2   1   6  -5   0
Prisons                   2      0   0  2   0   6  -6   0

Wafungaji:

2- Jerry Tegete (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Bakar Kondo (JKT Ruvu)
1- Abdul Banda, Jerry Santo (Coastal Union), Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan, Simon Msuva, Didier Kavumbagu (Yanga), Saad Kipanga, Iman Joel (Rhino Rangers), Aggrey Morris, Gaudencia Mwaikimba, Seif Abdallah (Azam), Laurian Mpalile (Prisons-OG), Elias Maguli, Jerome Lembeli, Shaaban Susan (Ruvu Shooting), Yusuph Machonge (Oljoro-OG), Juma Liziu, Masoud Ally (Mtibwa Sugar), Shaaban Juma (Ashanti Utd), Paul Nonga, Steven Mazanda (Mbeya City), Fully Maganga (Mgambo JKT), Haruna Chanongo (Simba), Salum Machaku, Husseni Bunu na Emmanuel Switta (JKT Ruvu)

No comments:

Post a Comment